Friday, December 30, 2016

Yamoto BandFt. Zena Mama lyrics

[Intro – Zena]
Tunaambaa ambaa ambaa na pwani yetu eh
Tunaambaa ambaa ambaa na pwani yetu eh
Zena, Yamoto Band twafanya yetu eh
Zena, Yamoto Band twafanya yetu eh
[Verse 1]
Umenifunza baya na zuri, kipi mi sijasikiaga
Ukanipaga na ushauri uweze kunisaidiaga
Zile teteme nteteme hutaki kuzisikiaga
Nipambane, niweze kukusaidia mama ai
Yalionikuta eh (naiona ngoma leo)
Oh mama eh (naiona ngondoo mie)
Mama dunia sio mbaya mama (naiona ngoma leo)
Oh binadamu mama (naiona ngondoo mie)
Ah mtoto, mtoto
Mi kwako bado mtoto
Usitishwe na miko, yamenishinda nimekuja kwako
Mama oh mameeh
Mama oh mameeh
Mwanao nimekua eh, najionea eh
Mama oh mameeh
Mama oh mameeh
Yale ya dunia eh, ulioniambia eh
Aaha
Umenifunza ah, kuna kovu na ndui
Kuna masika na vuli, ndimu sio chungwa
Kuna maziwa na tui, mh mmh
Pia simba na chui
Aee mamee, muda mwingine najisaidia
Hauchoki kufua, mama
Aee mamee, muda mwingine nakuudhi pia
Haukunichukia
Aiya mama
Ni kipi nikufanyie, sikioni mie
Ni kipi nikutendee? sijaona mama
[Chorus]
Ah ninavyokupenda mama eh
Anaejua ni Mungu
Ninavyokupenda mama
Anaejua ni Mungu
[Zena]
Ninavyokupenda mwanangu
Anaejua ni Mungu
Ninavyokupenda mwanangu
Akulinde mwanangu
[Verse 2]
Usiku ukifika ulikuwa uki-force mapema mi nilale
Hutaki nikeshe wakati kesho inabidi niende shule
Usiku ukifika ulikuwa uki-force mwanao mi nilale
Hutaki nikeshe wakati kesho inabidi niende shule
Mama, uligombana na majirani
Sababu mimi, kunitetea hata kama kosa nafanya mimi
Cha kukulipa mimi sioni, hapa duniani
Nakuombea uishi miaka mingi we mummy
Nafurahia, najivunia
Uwepo wako we kwenye dunia
Nakuombea, miaka mia
Uishi nisije potea njia
Na nafurahia, najivunia
Uwepo wako we kwenye dunia
Nakuombea, miaka mia
Uishi nisije potea njia, mama wee
[Zena]
Mama dhahabu alonipa baba yako
Miezi tisa umekaa tumboni mwangu
Furaha yangu kukuona machoni mwangu
Kila kukicha, kila kukicha namuomba Mungu
Kila kukicha, kila kukicha akulinde mwanangu
Mama eeh
Naogopa kupotea, we mama
Naogopa kupotea (nisije kukosa radhi)
Naogopa kupotea, we mama
Mama yangu! Oh
Naogopa kupotea, we mama
Naogopa kupotea (nisije kukosa radhi)
We mama eh, ah aa mama yangu oh
Mama nimekosea wapi ninachotaka nitambue
Mama nimekosea wapi nachotaka mi nijue
Mama nimekosea wapi ninachotaka nitambue
Mama nimekosea wapi nachotaka mi nijue
[Chorus]
Ah ninavyokupenda mama eh
Anaejua ni Mungu
Ninavyokupenda mama
Anaejua ni Mungu
[Zena]
Ninavyokupenda mwanangu
Anaejua ni Mungu
Ninavyokupenda mwanangu
Akulinde mwanangu
[Outro – Zena]
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh
Aah, uchungu wa mwana naujua mwenyewe
Aah, raha tumbo kuliona eh

No comments:

Post a Comment