Friday, December 30, 2016

Barakah Da Prince Siwezi LYRIC

[Verse 1]
Ulinipa donda ndugu
Donda ndugu ni gumu kupona
Ila siwezi sema sitopenda, nitamkufuru Mola
Unajua umenipa maumivu sugu
Maumivu sugu yasokwisha yote
Sababu ya kukupenda wee
Na sintochoka kukuombea kwa Mola
Akuzidishie baraka
Hata kukupenda wewe sichoki ii
Najua kunipenda sio lazima
Siwezi kuijenga chuki
Maa’ke najua
Nilijipa imani mwenyewe ipo siku utanithamini
Ila haukuwa nafasi yangu wewe
Naamini haukuwa fungu langu
Aaah kungoja yote kwanini?!
Leo, moyo wangu naukanda mie!
[Chorus]
Sitopunguza mapenzi (kwa we)
Kukuchoka siwezi (je we?)
Japo nimekosa penzi (nawe)
Nitaufariji moyo
Sitopunguza mapenzi (kwa we)
Kukuchoka siwezi (je we?)
Japo nimekosa penzi (nawe)
Nitaufariji moyo
Ooh mama wee
Naumia sana moyoni wee
[Verse 2]
Umenipa msiba
Msiba msiba bila kilio
Umenivua utu uzima
Nikatoa machozi ka ya mtoto
Hata kama nikisema nipende kwingine tatizo ni moyo
Moyo, kwana unaona nitadanganya
Tatizo uliopenda ni moyo
Siwezi kubishana nawe
Japo nafasi yangu kwako haikupatikana
Ila hongera kwa kuchukua usingizi wangu
Nashukuru mapema nilijua ipi nafasi yangu
Wewe sio mangapi ila nimeamua kuwapisha wenzangu
Na kujipa imani moyo wangu hutokusahau
Wewe, haukuwa nafasi yangu wewe
Naamini haukuwa fungu langu
Aaah kungoja yote kwanini?!
Leo, moyo wangu mi naukanda mie!
[Chorus]
Sitopunguza mapenzi (kwa we)
Kukuchoka siwezi (je we?)
Japo nimekosa penzi (nawe)
Nitaufariji moyo
Sitopunguza mapenzi (kwa we)
Kukuchoka siwezi (je we?)
Japo nimekosa penzi (nawe)
Nitaufariji moyo
Sitopunguza mapenzi (kwa we)
Kukuchoka siwezi (je we?)
Japo nimekosa penzi (nawe)
Nitaufariji moyo
[Outro]
Eeh usining’ang’anie mie, mie
Sipunguzi mapenzi
Eeh sipunguzi mapenzi

No comments:

Post a Comment