Friday, December 30, 2016

Fid Q Propaganda LYRIC

[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda
[Verse 1]
Machungu unapozimwa, ili ufunikwe na asiyeweza
Mbaya zaidi wanampa promo lakini kwenye shoo nammeza
Hautaki kuwa tatizo sababu unaeza tatuka
Huwezi kujua wapi ntatua ka jiwe gizani likitupwa
Wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua
Hamkomi, igeni nione jinsi msamba mnaupasua
Hivi unaishi ili ule, au unakula ili uishi
Kumbuka a small lake will sink a ship
Mazingira hatarishi, mabwana afya wana pesa mob
Uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo
Ogopa kuoa haraka kama unaogopa taraka
Na uki-vote in a hurry jua una produce corruption
Maneno yao matamu, midomo yao inanuka
Ukipewa usisahau, ukitoa toa bila kukumbuka
Usiohofie kupitwa ili mradi muda haukuachi
Amini kesho itafika kama ipo ili uipate
Tunachukiana kwa sababu tunaogopana
Tunaogopana kwa sababu hatujajuana
Hatujuani kwa sababu tunatengana
Dunia ni nzuri walimwengu hawana maana
[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda
[Verse 2]
Polisi huniita mzurulaji na wanajua mi ni emcee
Kisha hunipa ishara ka wanavuta radi kwa tasdii
Baya lisilonizuru ni jema lisilo na faida
Nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha
Kuanzia kata, tarafa, wilaya, mikoa hadi ngazi ya taifa
Nikifa siachi skendo, na uhakika ntaacha pengo
Hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu
Pia ni kama live direction, struggle machoni mwa Chegu
Ukiwa mkali ka Marco Chali, raia wata-feel tu
Wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu
Urafiki sio urafiki usipochanganywa na kazi
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi
Hupaswi kumuamini muongo hata kama ataongea ukweli
Dhambi kutumia dini kama njia ya kutapeli
Wanajiingizia kipato kwa kivuli cha misaada
Hawatufunzi tuwe viongozi, labda viongozi wa kuwafata
Utata huja tunapoanza kuwachunguza
Badala ya kuwafuata ndipo siri zinapovuja
Tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga
Ukishindwa kujiendeshe ujue mwenyewe tu ulipenda
Kama umevutiwa na asali jiandae kumkwepa nyuki
Hauwezi kumtisha kwa mawe adui aliyeshika bunduki
Ni uchunguzi wa kisayansi ambao haukufanikiwa
Kama ng’ombe kula nyasi tu halafu akatoa maziwa
[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda

No comments:

Post a Comment