Friday, December 30, 2016

Christian Bella Ft Ommy Dimpoz Nani Kama Mama LYRICS

[Intro – Ommy Dimpoz]
Mama oh mama
Na Poz Kwa Poz!
Mama oh mama
Nani kama mama
[Verse 1 – Christian Bella]
Oh yah nani kama mama, heshima kwa mama
Yale mateso ulinibeba miezi mitisa tumboni mwako
Pole sana mama
Nikupe nini? Heshima kwa mamaaa (maama ee)
Uliteseka siku ya kunitoa duniani
Nikupe nini? (mama eeh)
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa
[Chorus – Christian Bella]
Mama ee
Nani kama mama aaa? (mama mama)
Nani kama mama aaa? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama aaa? (usipotoke umdharau mama yoyo)
Nani kama mama aaa? (ma ma ma mama)
[Verse 2 – Ommy Dimpoz]
Hello mama, hii ni kwako mama
Si, nimekukumbuka sana (mama)
Usiku na mchana, ai
Nakuombea upumzike salama eh
Tabia na heshima eh, busara na hekima eh ae
Ulinifundisha vyema eh, si, nakuombea upumzike salama
[Bridge – Ommy Dimpoz]
Matatizo ya dunia, kweli ninayapitia
Yale ulionihusia eeh, ya kweli mama ee
Matatizo ya dunia, kweli ninayapitia
Yale ulionihusia eeh, eee mama eeh
[Verse 3 – Christian Bella]
Malezi ya mama, elimu ya mama
Haina ada wala cheti ila ni zaidi ya elimu ya chuo kikuu
Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikilia usiku mama lazima utakesha na mimi
Huwezi kukubali niwe macho usiku
Nawe ufumba macho yako
Mapenzi ya maaama kwa mtoto wake haina mfano
Hata mapenzi ya boyfriend na girlfriend hayafiki hata robo
Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikiumwa usiku mama lazima utakesha na mimi
Mola wasaidie wakina mama wote
Wape maisha marefu, nani kama maama?
Mama ni maama yeeye
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa
Mama maama yeee, mama na mama
Nasema mama ni mama yee
Nani kama mama? (mama)
Mama ni mama (mama)
Heshima kwa mama
Mama ni mama
Wee!
[Chorus – Christian Bella]
Ma ma!
Nani kama mama aaa? (mama mama)
Nani kama mama aaa? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama aaa? (usipotoke umdharau mama yoyo)
Nani kama mama aaa? (ma ma ma mama)

No comments:

Post a Comment