Friday, March 17, 2017

MUSIC: BARAKA DA PRINCE – ACHA NIENDE (LISTEN/DOWNLOAD)

MUSIC: BARAKA DA PRINCE – ACHA NIENDE (LISTEN/DOWNLOAD)
Baada ya ngoma ya Nisamehe ambayo alimshirikisha Alikiba kufanya poa kias chake, Baraka Da Prince ameamua kuja na hii hapa mpya kabisa ambayo kaipachika jina la Acha Niende. 
Producer wa ngoma ni Bob Manecky. Enjoy nayo kwa kuisikiliza na hata kuidownload kupitia Widget hii hapa chini.
https://www.audiomack.com/…/parfe…/acha-niende-perfect255com
https://www.audiomack.com/…/parfe…/acha-niende-perfect255com





Alikiba leo kutumbuiza kwenye SXSW Music Festival

Alikiba leo kutumbuiza kwenye SXSW Music Festival, Texas akiwa na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black.
Alikiba, Ijumaa hii ataungana na mastaa mbalimbali kutoka pande tofauti za duniani kutumbuiza kwenye tamasha kubwa liitwalo, SXSW Music Festival.
Tamasha hilo linafanyika kwa siku kadhaa huko Austin, Texas nchini Marekani. Alikiba ni sehemu ya orodha iliyopendekezwa na tamasha jingine la Passport Experience (litafanyika Septemba 3, Atlanta, GA) lililoanzishwa na Akon pamoja na meneja wa Ludacris, Chaka Zulu.
Kwenye orodha hiyo, Kiba anaungana na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black pamoja na msanii wa Nigeria, May D. Wengine ni pamoja na Karlon, Fully Focus na DJ WaxFiend.
SXSW Music Festival ni moja ya matamasha makubwa zaidi duniani ambalo hufanyika kila mwezi March huko Austin, Texas.
“Each year the SXSW Music Festival hosts a comprehensive mix of brand new, up-and-coming, international, and legendary artists performing in bars, clubs, parks, churches, hotels, and just about everywhere else you can imagine around Austin, Texas,” yanasema maelezo yake.




Tuesday, March 14, 2017

Alikiba amefunguka kwa kukanusha taarifa ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana mpango wa kufanya kolabo na Justin Bieber.
Akiongea na mtangazaji wa JEMBE FM JJ akiwa Las Vegas Marekani, Alikiba alidai taarifa za kwamba ana mpango wa kufanya kolabo zitungwa na mashabiki wake wa muziki.
“Ni mashabiki waliamua kuzusha, kwa hiyo ni vitu vya uzushi havina maana,” alisema Alikiba.
Pia muimbaji huyo alidai hana mpango wakufanya kolabo na Wizkid kwa sasa lakini ukifika muda na akipata nafasi anaweza kufanya hivyo.
Baraka Da Prince ni msanii ambaye alikuwa akionekana kuwa karibu sana na msanii mwenzake Alikiba .
Perfect crispin imeamua kupiga story na meneja wao katika lebo ya Rockstar4000 Seven Mosha
“Hamna distance baina ya Baraka na Alikiba, katika lebo yetu kila msanii anajitegemea, Baraka hivi sasa  yuko katika harakati za kumaliza album yake, pia ana shows zake ambazo anapiga ndio maana hamuoni ukaribu.” ALisema Seven Mosha.
Alikiba akamilisha collabo na malkia wa Afrika
Kwa upande wa Alikiba ameonesha kuwa na furaha kuweza kupata nafasi ya kufanya kazi na mkongwe huyo katika muziki ambaye ameshafanya mambo mengi kupitia muziki wake barani Afrika, hivyo Alikiba alishukuru kuweza kukamilisha kazi hiyo.
"Last night final recordings with Mama Yvonne Chakachaka . I am honored and truly excited about our project . Thank you Mama for everything" aliandika Alikiba
Lakini kwa upande wa Yvonne Chaka Chaka pia ameonesha kufurahishwa na uwezo wa Alikiba na kuipenda kazi yao hiyo ambayo tayari, pia Yvonne Chaka Chaka ameshukuru kuweza kupata nafasi ya kufanya kazi na Alikiba kutoka Tanzania.
"Learning Swahili words. Thank u Ali. Kiba. I love the song. Yes u are a good Son. Thank you to the  'A' team" aliandika Yvonne Chaka Chaka
Kwa upande wa Alikiba hii itakuwa ni collabo ya tatu ya wasanii kutoka nje ya Tanzania,  Collabo ya kwanza ilikuwa na kundi la Sauti Soul kutoka nchini Kenya ambao walitoa wimbo wa "Unconditionally Bae", collabo ya pili kwa Alikiba ni AJE Remix ambayo amefanya na rapa M.I kutoka Nigeria, na collabo ya tatu ambayo tayari ameiweka wazi ni ni Alikiba na Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.
Sijaona wakumlinganisha na Alikiba - Harmorapa
Rapa ambaye amejizolea umaarufu sana kupitia mitandao ya kijamii Harmorapa amefunguka na kusema kwa Tanzania hii hajaona msanii wa kumfananisha na Alikiba na kusema hata ngoma yake ambayo amefanya na Juma Nature alitaka kufanya na Alikiba.
Harmorapa anasema kabla ya kurekodi ngoma yake hii mpya ambayo amefanya na mkongwa Juma Nature alijitahidi sana kumtafuta Alikiba ili aweze kufanya naye lakini jitihada zake ziligonga mwamba kutokana na ukweli kwamba Alikiba alikuwa na mambo mengi na kushindwa kumfikia kuzungumza naye jambo hilo.
"Kiukweli King Kiba kwa Tanzania hapa sioni wa kumfananisha naye, kwa hiyo nisema sijaona bado wa kumlinganisha naye sababu jamaa anafanya vizuri sana na anajua muziki sana, hata kabla ya kurekodi hii kazi yangu mpya nilifanya jitihada na watu wa karibu na Alikiba japo niweze kufanya naye kazi lakini sikuweza kufanikiwa kutokana na mambo yake kuwa mengi sana na watu pia ambao walikuwa wakinipa connection naye kuna vitu sikuweka sawa, na muda nikaona unazidi kwenda nikasema ngoja nifanye tu" alisema Harmorapa