Alikiba akamilisha collabo na malkia wa Afrika
Kwa upande wa Alikiba ameonesha kuwa na furaha kuweza kupata nafasi ya kufanya kazi na mkongwe huyo katika muziki ambaye ameshafanya mambo mengi kupitia muziki wake barani Afrika, hivyo Alikiba alishukuru kuweza kukamilisha kazi hiyo.
"Last night final recordings with Mama Yvonne Chakachaka . I am honored and truly excited about our project . Thank you Mama for everything" aliandika Alikiba
Lakini kwa upande wa Yvonne Chaka Chaka pia ameonesha kufurahishwa na uwezo wa Alikiba na kuipenda kazi yao hiyo ambayo tayari, pia Yvonne Chaka Chaka ameshukuru kuweza kupata nafasi ya kufanya kazi na Alikiba kutoka Tanzania.
"Learning Swahili words. Thank u Ali. Kiba. I love the song. Yes u are a good Son. Thank you to the 'A' team" aliandika Yvonne Chaka Chaka
Kwa upande wa Alikiba hii itakuwa ni collabo ya tatu ya wasanii kutoka nje ya Tanzania, Collabo ya kwanza ilikuwa na kundi la Sauti Soul kutoka nchini Kenya ambao walitoa wimbo wa "Unconditionally Bae", collabo ya pili kwa Alikiba ni AJE Remix ambayo amefanya na rapa M.I kutoka Nigeria, na collabo ya tatu ambayo tayari ameiweka wazi ni ni Alikiba na Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment