Alikiba leo kutumbuiza kwenye SXSW Music Festival, Texas akiwa na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black.
Alikiba, Ijumaa hii ataungana na mastaa mbalimbali kutoka pande tofauti za duniani kutumbuiza kwenye tamasha kubwa liitwalo, SXSW Music Festival.
Tamasha hilo linafanyika kwa siku kadhaa huko Austin, Texas nchini Marekani. Alikiba ni sehemu ya orodha iliyopendekezwa na tamasha jingine la Passport Experience (litafanyika Septemba 3, Atlanta, GA) lililoanzishwa na Akon pamoja na meneja wa Ludacris, Chaka Zulu.
Kwenye orodha hiyo, Kiba anaungana na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black pamoja na msanii wa Nigeria, May D. Wengine ni pamoja na Karlon, Fully Focus na DJ WaxFiend.
SXSW Music Festival ni moja ya matamasha makubwa zaidi duniani ambalo hufanyika kila mwezi March huko Austin, Texas.
“Each year the SXSW Music Festival hosts a comprehensive mix of brand new, up-and-coming, international, and legendary artists performing in bars, clubs, parks, churches, hotels, and just about everywhere else you can imagine around Austin, Texas,” yanasema maelezo yake.
No comments:
Post a Comment