Alikiba amefunguka kwa kukanusha taarifa ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana mpango wa kufanya kolabo na Justin Bieber.
Akiongea na mtangazaji wa JEMBE FM JJ akiwa Las Vegas Marekani, Alikiba alidai taarifa za kwamba ana mpango wa kufanya kolabo zitungwa na mashabiki wake wa muziki.
“Ni mashabiki waliamua kuzusha, kwa hiyo ni vitu vya uzushi havina maana,” alisema Alikiba.
Pia muimbaji huyo alidai hana mpango wakufanya kolabo na Wizkid kwa sasa lakini ukifika muda na akipata nafasi anaweza kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment