Tuesday, April 17, 2018

Ray C - Na wewe Milele

Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Siku niliyokuona macho yangu yalishtuka
Nilijua roho yangu mimi kwako imefika
Na sasa tupo pamoja uwe wangu niwe wako
Kwa shida na raha zote moyo wangu uko kwako
Na raha zako siwezi mimi kwako kuzikosa
Na raha zako siwezi mimi kwako kuzikosa
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Penzi sitolibadili kwa udi hata ubani
Penzi letu liwe tamu, tamu lishinde asali
Mpenzi usinidhulumu nipe raha za ndani zote
Ziishi moyoni mwangu milele hata milele
Ziwaudhi maadui wasopenda penzi letu
Ziwaudhi maadui wasopenda penzi letu
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Kila kukicha natabasamu
Nina furaha kuwa na wewe
Wanipa raha bila karaha
Mimi na wewe furaha tele
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja
Nataka niwe na wewe milele
Nataka tuwe na watoto baby
Nataka tuishi wote pamoja

Stamina ft Jux - Alisema

It’s Moro Town baby
You know what Kev
This is so conscious man
Sio kila Mchaga muuza duka so nisiogope kuitwa Mangi
Kupanda na kushuka ndio chart isiyohitaji rangi
Bora kuitwa mshamba kwenye group la matapeli
Subira ikikosa kamba jipange kuivuta heri
Alisema nisilete uchizi mbele ya daktari wa akili
Nisiwe na hasira za mkizi ili mvuvi anifanye dili
Kukosa na kupata ndo mechi isiyokua na draw
Kama maisha karata mchangaji nimkabe koo oh
Madawa ya kulevya niogope yatanipa uchizi
Maishani nisiwe dereva kwenye basi la wazinzi
Kengeza ndo macho yangu nisimcheke mwenye chongo
Nipendezeshe maisha yangu ka dressing table ya Mkongo
Nisile ada kisa demu mapenzi hayana mradi
Maisha ni PS game hayachezeki bila pad
Elimu ya mtaani niijue ili nikuze ukoo
Ila elimu ya darasani nisihitimu bila ya joho
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Usoni nisi-pretend ugumu wakati moyoni nina usharo
Gangsta sio kuvuta ndumu nijipange nitafute miparo
Kama pesa hazilali mtafutaji nisichonge kitanda
Asali ikiwa juu ya dari mrinaji nisichome kibanda
Alisema mjini mipango sio urefu wa magorofa
Samaki akiliwa na chambo nijue mvuvi ameshaanza urofa
Nisinywe gongo na biskuti nikadhani ndio janja teja
Nikaze buti ili niji-boost wapinzani wasiniite kinega
Kama muda ni pesa nifungue account ya saa
Nisiseme boom linatesa huku principle anashinda bar
Maisha trailer za Kanumba nsiogope kufa kiuongo
Mimba ya ujinga haina mkunga nitafute ujanja kwa usongo
Nisimdharau fukara kisa nimemzidi kipato
Mtoto nisimfanyie tohara akikua aniite Pilato
Fisadi akiwa jogoo tetea nitafute kambi
Mziki una kwashiorkor nsiache hadi unipe kitambi
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Nisishangae kukuta bwanga kwenye chumba cha ma-model
Ila nishangae kuziona shanga kwenye kiuno cha mtoto mdogo
Kipimo cha utapeli hakipimwi na mzani wa ubongo
Nsibishane na ukweli ikiwa nina chembe za uongo
Mfupi ndio aliyegundua ngazi ili mradi apate virefu
Nisimtukane mzazi nitapata radhi ya ukosefu
Selemara rudi VETA mende akiangusha kabati
Daudi akipigwa ngeta nijue kesi kwa Goriati
Primary na shule ya msingi zina utofauti wa kimasilahi
Inabidi nione vifo vingi ili nijue thamani ya uhai
Nguvu za uongo wa video zisinipotezee ujana
Nisijiite jembe huku kimeo wakati pabichi nakwama
Nikikosa fasta nitubu masizi yasigeuke kiwi
Na nisiogope kuitwa bubu kwenye kundi la viziwi
Nisi-force penzi kwa changu ni bora nikatumia Detto
Na Moro ndio mkoa wangu nikiukana wataniita Petro
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Uwezo nnao alisema
Niachane nao alisema
Kama Mungu alitoa tusishangae anapotwaa
Amini kila binadamu alizaliwa shujaa
So this one is dedicated to all who lost their beloved ones

Kwenu Vipi by Stamina ft Ney Wa Mitego

Mziki wenu ana ana doo
Unafanya mshindwe hata kufikiri
Kutwa kwenye vioo kuliko kuandika mashairi
Hip Hop mizuka yakujuza usivyojua
Hivi mziki wenu unanuka
Mbona mnabana pua
Swali lako kwangu halina jibu
Ulichouliza hakinihusu
Sema kama unanijaribu au dogo una-force beef
Hapa kwangu pakavu sitaki upuuzi
Maswali ya kupana pua na poda muulize Dimpoz
Aa haa hamna cha maana kutwa kuwaimbia wasichana
Unalikuta libaba lizima eti oh nakula ujana
Haziingii akilini na hazielimishi jamii
Sa nimjue wa nini aliyemwaga pombe ya nanii Eeh
Okay Professor Jay bwana mdogo si unamjua
Hata baba ‘ako nyumbani naimani anamtambua
Kwa nyimbo za kuelimisha we pimbi kaa kimya
“Kamili Gado” imetoboa ali-change mtu mzima
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu safi
Huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi
Mnajifanya mnafanya ngumu wakati hamna majukumu
Wengi wenu wala ndumu na bado mnaishi kwenu
Usibishane na mimi kwanza we bado unasoma
Shoo zenu bei rahisi hata kwa bia nyie mnafanya
Hip Hop inahitaji kichwa sio kunywa mchuzi wa pweza
Blaza huku kwetu ulifichwa umesepa sababu ya kumezwa
Ama kweli nimeamini wanawake mkiwezeshwa mnaweza
Kama umenishindwa mimi je Fid Q utamuweza
Kwanza hamtambui kwamba huu mziki ni kazi
Na ndo maaana mnakatazwa na wazazi
Unafanya mziki mwaka wa kumi huna hata bajaji
Nyie sio wasaniii ni wasindikizaji
Huko kwenu mnajua waganga sababu mnapeana stress
Ndo maana hadi nyimbo vamba mtaani zinakuwa the best
Blaza ushaachia siti so punguza kujisifu
Huku viumbe tunaachia hit bila hata kumtaja Chief
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu safi
Huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi
Kwa ku-post picha Insta hilo mnaongoza
Utasikia huu mjengo wangu mpya kumbe umepanga unajiongeza
Nasikia daily mko gym eti mnatanua vifua
Wakati mkirudi makwenu wengi wenu mnajichubua
Ebo
Mnajifanya mnakaza huku mnakufa njaa
Hakuna mnachopata zaidi ya sifa kwenye mitaa
Kwanza mnatudhalilisha kutwa mnapiga vizinga
Umarekani mwingi mpaka mnakula unga
Si bora sisi unga kuliko nyie mapu***
Hana style hamna swagg wala hamjui kutunga
Kwa kuongeza sifuri kwa hilo mnaujasiri
Hata video ya milioni 2 utasikia milioni 200
Sh*t
Bwa’ mdogo ongea na mimi mbona unawasema watu
Wataje kwa majina ka kweli unafanya Hip Hop
Kwanza umekula au unaanzisha tu mgogoro
Kabla hatujafika mbali una nauli ya kurudi Moro
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi
Aah huku kwetu safi
Huko kwenu vipi
Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi
Anha kama hupati unachopenda
Penda unachopata au sio
Mwisho wa siku hii ni biashara
Inabidi mwisho wa siku tupendane sisi kwa sisi
Au sio
Don’t take it personal man
(Seductive Records)
Au sio Mambo yataongeleka au sio
Tutagombana mwisho wa siku Bongo Flava na Hip Hop
We all teame
Stamina Nay Wa Mitego T-Touch au sio
Take it easy homeboy don’t panic
It’s just a business man
Calm down errbody
Hahaha napenda nachokisikia
I’m out

Sam sina raha

Kila siku mi naumia na mawazo wapi nitampata mkee mwema maishani Najifuta machozii Nikasahau nilivyo tendwa zamani
Naona kama ngege waa moto mazuri kuwa nawe maishani Nacho mwambia ananielewaa Napenda animpenda Sito mwaacha asilani Gari pesa sinaa Ndio maana nakuita mchuba We wa gari na nyumba ama pesa ndio chumba Bora unieleze mchumba Mi si mgeni wa mpenzi mwenzako Maumivu naya tambua Nipe nikupu ndio ishara ya upendo Haiwezekani daily unanizingua Nisipokuona sina raha eeh Naumia namawazo Sema Kama haunipendi Ikiwa haunipendi Haiwezekani we daily unanizingu We nimgonjwa na unamwitaji mtabibu Mi ni daktari ki maradhi ntakutibu

Dully Sykes - Baby Candy

Baby usilie
Mi najua wazo lako
Ni kuwa na mimi leo mpaka kufa (baby Candy usilie)
Nenda shule kwanza
Halafu mambo ya love ndo baadae yatafuata
Usione nadharau
Hata mimi nakungoja baby Candy
Wala sijakusahau
Bado nakupenda usione sikupendi (baby usilie)
Umetoroka kwenu
Umenifuata home
Usiniponze Candy
Rudi kwenu Dom
Unataka tu-spend jigi, hug na rom
U-study mapenzi yatazidi ka ya dili ya niko
Kwa mwingine siendi
We ni zaidi ya utamu
Na ngoja ufike age
Mpaka moya msimamu
Itakuwa afadhali, rahisi kuja kwangu kwa room
Pia uache tabia zako za kutaka kunywa sumu
Nayafuta machozi
Acha kulia Candy
Nitakupa mapenzi
Utapokuwa na age
Takua upate umri wa ku-spend na mi
Usije ukanifungisha nikashangaza jamii
Baby usilie
Mi najua wazo lako
Ni kuwa na mimi leo mpaka kufa (baby Candy usilie)
Nenda shule kwanza
Halafu mambo ya love ndo baadae yatafuata
Usione nadharau
Hata mimi nakungoja baby Candy
Wala sijakusahau
Bado nakupenda usione sikupendi (baby usilie)
Sio kwamba sikupendi
We bado mdogo sana
Sikia baby Candy
Mi nakupenda sana
Nangoja ukue kwanza
Twaweza kuoana
Nataka niwe wa kwanza
Kikombe kukivunja
Wacha kulia sana
Unanisononesha
Mi nakusihi sana
Pia nakukumbusha
Rudi shuleni soma
Kwani bado mapema
Usije pata homa
Kwa kuniwaza mama
Hata rafiki zangu
Watanitenga pia
Na itakuwa kashfa kwangu
Hata kwako pia dear
Nadhani umenisikia
Yote nilokwambia
Wacha kulia lia
Wacha kulia lia
Baby usilie
Mi najua wazo lako
Ni kuwa na mimi leo mpaka kufa (baby Candy usilie)
Nenda shule kwanza
Halafu mambo ya love ndo baadae yatafuata
Usione nadharau
Hata mimi nakungoja baby Candy
Wala sijakusahau
Bado nakupenda usione sikupendi (baby usilie)
Baby Candy
Si kwamba sikupendi
Nangoja ukue, umalize shule
Tuta-spend, tuta-spend
Baby usilie
Mi najua wazo lako
Ni kuwa na mimi leo mpaka kufa (baby Candy usilie)
Nenda shule kwanza
Halafu mambo ya love ndo baadae yatafuata
Usione nadharau
Hata mimi nakungoja baby Candy
Wala sijakusahau
Bado nakupenda usione sikupendi (baby usilie)

Sizonje - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro

Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Tulikaa barazani tukasikia kelele
Kelele toka ndani mtu anaruka dirishani
Sizonje karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu
Karibu sana Sizonje hii ndo nyumba yetu
Tulipoficha mundu za kupondea wezi
Kwani makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne
Vitatu havifunguki kimoja hakina mlango
Japo kuwa kina watu ndani na hawaongei Kiswahili
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni
Huna haja ya kwenda kule kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa ‘Usiyemtaka Kaja’
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Najua wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje
Si unajua harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue
Sawa Sizonje huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini
Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana wana bahasha za khaki mikononi
Kama hamtupi taka shimo hili mlichimba la nini
Lakini pia kwenye sauti zao Sizonje
Kuna watoto wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa njoo nikuonyeshe huku uchochoroni
Uone maajabu mengine ya nyumba hii
Sizonje ukiona tembo anaringa
Ujue mvua zinakaribia
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone maajabu ya nyumba yetu

Hafsa ft Banana Zorro Pressure

Mpenzi wangu mimi kweli nakupenda
Unajua ndo maana wanitesa
Sio siri honey wanipa pressure
Pressure ah pressure
Pressure pressure pressure ya nini
Nakutesa tesa na nini
Pressure pressure pressure ya nini
Mbona mpenzi huniamini
Kila tunapotoka eh mi narudi na ndonya
Napigwa eti nawachukulia
Khadija ndio nani mbona anasumbua
Usiku hatulali simu kila mara
Sababu maneno maneno
Maneno yako mami
Sababu mdomo mdomo eh
Mdomo wako mami
Nisiongee na watu eh
Mbona wasichana pekee
Labda ni madada zangu eh
Mbona mabusu tele
Mambo ya kizungu
Maumaya sipumui akija
Hata huduma zinasitishwa
Niweke wazi
Mi naona mwenzangu huogopi maradhi
Mama mama hao wengine wadhamini eh
Mpenzi wangu mimi kweli nakupenda
Unajua ndo maana wanitesa
Sio siri honey wanipa pressure
Pressure ah pressure
Pressure pressure
Pressure ya nini
Nakutesa tesa na nini
Pressure pressure
Pressure ya nini
Mbona mpenzi huniamini
Vipi kuhusu Anitha
Yule binti wa Morocco oh
Acha yule Rose
Mwenye mtoto wako
Kitanda hakizai harumu
Ile kweli damu yangu (nisamehe)
Kuhusu huyo Anitha
Mh
Anitha mbona simkumbuki
Mbona kigugumizi
Sababu waniona mwizi
Mbona kigugumizi
Mapenzi yamekwisha siku hizi
Mpenzi wangu mimi kweli nakupenda
Unajua ndo maana wanitesa
Sio siri honey wanipa pressure
Pressure ah pressure
Pressure pressure
Pressure ya nini
Nakutesa tesa na nini
Pressure pressure
Pressure ya nini
Mbona mpenzi huniamini
Nakupenda nakuheshimu lakini huna aibu wewe
Nakupenda nakuamini lakini sina imani tena nawe eh
Kama zamani na sasa kuna tofauti nisamehe
Kama zamani na sasa kuna tofauti tumalize
Tofauti zetu eh
Mimi na wewe eh
Tofauti zetu eh
Mpenzi wangu mimi kweli nakupenda
Unajua ndo maana wanitesa
Sio siri honey wanipa pressure
Pressure ah pressure
Pressure pressure
Pressure ya nini
Nakutesa tesa na nini
Pressure pressure
Pressure ya nini
Mbona mpenzi huniamini
Allan Mapigo Said Komorien
Banana ananitesa eh
Hey

AbduKiba Bayoyo lyrics

Habibty habibty wauba wangu wa ubani eh
Raha za ndani wewe umefunzwa na nani eh?
Mtoto mashaallah mtoto ma habuba
Mtoto Bilal Islat Naifat woyo oh oh
Yako majina yanantatiza bwana
Kila kukicha afadhali lile la jana
Habibty oh-oh habibty wewe
Wangu mimi kwako wewe kudunda dunda kwako
Kudunda dunda nami
Habibty mashaallah umezaliwa Tanga kisiwani
Napenda zile dimpose napenda zile njozi zako za usiku
Aah aah
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Cheza na mimi (bilinge bwa bilinge bwa bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Cheza na mimi (bilinge bwa bilinge bwa bilinge bwa)
Nafuraha tele kuwa na wewe
Siwezi kukukata kwenye maisha furaha yangu
Nyota yangu kizimwe changu nyumba yangu
Habibty wee iih
Ni wengi wenye mapenzi
Nishasemwa sana juu yako kwa vile mi unanienzi
Mapenzi real real real na kukuacha mimi siwezi
Hiyo ni ndoto ya mapenzi kwangu wa pekee
Napenda zile dimpose napenda zile njozi zako za usiku
Aah aah
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Cheza na mimi (bilinge bwa bilinge bwa bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Baby bilinge bayoyo (bilinge bwa)
Cheza na mimi (bilinge bwa bilinge bwa bilinge bwa)
Alekufunza habibty mahaba tusije saliti
Mungu wa raha na dhiki (mahaba) habibty bilinge yo
Alekufunza Habibty mahaba tusije saliti
Mungu wa raha na dhiki habibty bilingeba
Habibty yoyo oh oh oh
Habibty wewe mamaa
Habibty yeeeh njoo!