Tuesday, April 17, 2018

Stamina ft Jux - Alisema

It’s Moro Town baby
You know what Kev
This is so conscious man
Sio kila Mchaga muuza duka so nisiogope kuitwa Mangi
Kupanda na kushuka ndio chart isiyohitaji rangi
Bora kuitwa mshamba kwenye group la matapeli
Subira ikikosa kamba jipange kuivuta heri
Alisema nisilete uchizi mbele ya daktari wa akili
Nisiwe na hasira za mkizi ili mvuvi anifanye dili
Kukosa na kupata ndo mechi isiyokua na draw
Kama maisha karata mchangaji nimkabe koo oh
Madawa ya kulevya niogope yatanipa uchizi
Maishani nisiwe dereva kwenye basi la wazinzi
Kengeza ndo macho yangu nisimcheke mwenye chongo
Nipendezeshe maisha yangu ka dressing table ya Mkongo
Nisile ada kisa demu mapenzi hayana mradi
Maisha ni PS game hayachezeki bila pad
Elimu ya mtaani niijue ili nikuze ukoo
Ila elimu ya darasani nisihitimu bila ya joho
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Usoni nisi-pretend ugumu wakati moyoni nina usharo
Gangsta sio kuvuta ndumu nijipange nitafute miparo
Kama pesa hazilali mtafutaji nisichonge kitanda
Asali ikiwa juu ya dari mrinaji nisichome kibanda
Alisema mjini mipango sio urefu wa magorofa
Samaki akiliwa na chambo nijue mvuvi ameshaanza urofa
Nisinywe gongo na biskuti nikadhani ndio janja teja
Nikaze buti ili niji-boost wapinzani wasiniite kinega
Kama muda ni pesa nifungue account ya saa
Nisiseme boom linatesa huku principle anashinda bar
Maisha trailer za Kanumba nsiogope kufa kiuongo
Mimba ya ujinga haina mkunga nitafute ujanja kwa usongo
Nisimdharau fukara kisa nimemzidi kipato
Mtoto nisimfanyie tohara akikua aniite Pilato
Fisadi akiwa jogoo tetea nitafute kambi
Mziki una kwashiorkor nsiache hadi unipe kitambi
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Nisishangae kukuta bwanga kwenye chumba cha ma-model
Ila nishangae kuziona shanga kwenye kiuno cha mtoto mdogo
Kipimo cha utapeli hakipimwi na mzani wa ubongo
Nsibishane na ukweli ikiwa nina chembe za uongo
Mfupi ndio aliyegundua ngazi ili mradi apate virefu
Nisimtukane mzazi nitapata radhi ya ukosefu
Selemara rudi VETA mende akiangusha kabati
Daudi akipigwa ngeta nijue kesi kwa Goriati
Primary na shule ya msingi zina utofauti wa kimasilahi
Inabidi nione vifo vingi ili nijue thamani ya uhai
Nguvu za uongo wa video zisinipotezee ujana
Nisijiite jembe huku kimeo wakati pabichi nakwama
Nikikosa fasta nitubu masizi yasigeuke kiwi
Na nisiogope kuitwa bubu kwenye kundi la viziwi
Nisi-force penzi kwa changu ni bora nikatumia Detto
Na Moro ndio mkoa wangu nikiukana wataniita Petro
Alisema
Nifanye nachofanya bwana mimi nisizubae
Uwezo ninao alisema
Maneno yakisemwa wala mimi nisishangae
Niachane nayo alisema
Ubinadamu kazi alisema
Nisiwe na haraka na maisha alisema
Nisichague kazi alisema
Nakumbuka iye eh
Uwezo nnao alisema
Niachane nao alisema
Kama Mungu alitoa tusishangae anapotwaa
Amini kila binadamu alizaliwa shujaa
So this one is dedicated to all who lost their beloved ones

No comments:

Post a Comment