Saturday, April 14, 2018

Roma Zimbabwe lyrics

ROMA ZIMBABWE LYRICS

Wengi mlijiuliza walioniteka ni
maaskari?
Mkanitafuta vituo vyote Cetral hadi
sitaki shari,
Wakasema hawajui nilipo mama
alienda mpaka mochwari,
Daaah!,ya kaisari mwachie kaisari,
Machozi yenu yatalipwa mimi
nafunga na kusali
BRIDGE
Imba roma Imbaaa
Imba roma Imbaaa,
Imba roma Imbaaa,
VERSE 1
Mungu wa paul ndio mungu wadaudi,
Na ndio mungo wa John Mnaemuita
Yohana wa wayahudi,
Mwanangu alimuuliza mama “Baba
lini atarudi”?,
Na mke wangu aliwaliza
kuwashukuru sinabudi,
Kwa hamu ya kuwa mimi sio tu
rapper,
Mimi ni baba wa Familia,
Nawatoto mahitaji nawapa ka
isemavyo biblia,
Kipi bora?Nife mseme nilikufa
kiharakati?,
Siogopi kufa ila nawaachaje
wanaobaki?,
Je! Nani kati yenu mwanangu
atampa malezi?,
wapi atapata mahitaji?,wapi atapata
mapenzi?,
Mama nae wapi atapata mahitaji na
malezi?,
Na report ya upelelezi vipi akiiteka
mtekaji?,
Je! Kaburi langu mtalipalilia majani,
Nimeumwa hamjakuja
niona,mnangoja mje msibani?,
Nilipokuwepo sikuwa najua hii
sanne,hii saanane,
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu
zangu tuonane,
Nimechapwa Mijeledi nimevunjwa
bila huruma,
Asante mliopaza sauti nimeiona
nguvu ya umma,
Siku tatu nimefungwa macho,mikono
imefungwa nyuma,
CHORUS
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
BRIDGE
Imba roma Imbaaa,
Oo,Eee Roma(sema baba wewe)
VERSE 2
Nasimama na naunga hoja kwenye
uchumi wa Viwanda,
Nanasi linauza msoga,tikiti linaoza
shamba,
Walioniteka hawakuja na noah,Ni
uvumi na visanga,
ila kutekanateka huu ni uhuni wa
kishamba,
Weka Bunduki chini si tubishane kwa
hoja,
Maana sote lengo letu kuijenga
Tanzania moja,
Mi sikuona nyota kwa shoulder,Ila
najua wewe ni soldier,
(Inshallah)Ulikuja mwenyewe ama
ulipewa order(hewallah),

Aminini siku hazigandi,wewe ni
yanga mimi simba,
Kuwa mpinzani sio dhambi,
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani,
Simba akichukua kombe sijui
atapona nani,
Na kuna mbunge alisema eti
nimemtukana mkuu,
Utahukumiwa na mkono wa
Mungu,kumshtakia aliye juu,
Kwanza lini,na kwanini mimi
nimtukane mjomba,
Umepewa gari ya wagonjwa,mi
Tanga wananijalia bomba,
Mimi mbarikiwa na nikifa nitaketi
kuume kwa baba,
na ni mtu wa watu that is
why,lilisimama bunge la bajeti,
Kunijadili mtanzania kuwa makini
pia makinikia nayatungia,
Mapini Piyaa,
Nilitabiri utaitwa Raisi kipindi
unaitwa waziri,
Japo maisha sio rahisi ila pongezi
unastahili,
waliosadiki roma ataonekana kabla
ya jumapili,
God bless imetimia injili nilio itabiri,
CHORUS
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
BRIDGE
Imba roma(ee ee roma),
Zimbomboo we simama(ee ee
roma),
sema baba wewe(ee ee roma),
iyelelel mama wewee(zimbombo we
simama),
watakwenda,uko zimbabwee,
ee ee roma(iyelele mama wewee)

No comments:

Post a Comment