Leo nalivua pendo nililopenda zamani
Nabadilli wangu mwendo nami niwe furahani
Nimechoshwa na skendo, vita na purukushani
Kweli asiyejua pendo apendwapo hapaoni

Nilimpa kwa kishindo penzi lote la moyoni
Raha na wingi uhondo sikumnyima mwandani
Ameyavunja kwa nyundo mwenzenu sikuamini
Leo nalivua pendo nirudi yangu thamani

Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
Hatuwezi kulingana kauli hata matendo
Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo

Niliyajenga kwa nondo mapenzi yangu ya ndani
Kwa ufundi na miundo na mambo yote ya Pwani
Kumbe nalea uvundo aibu tupu nyumbani
Kweli asiyejua pendo hapendeki ni shetani

Pendo gani la magendo apendwae hafanani
Leo naliweka kando pendo hili la kihuni
Najiepusha na lindo kumlinda hayawani
Kwani mapenzi mkondo hayataki ushindani yeah

[Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
Hatuwezi kulingana kauli hata matendo
Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
Hatuwezi kulingana kauli hata matendo
Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
Ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
Hatuwezi kulingana kauli hata matendo
Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
Hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
Hatuwezi kulingana kauli hata matendo
Kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
Nimehitimu msondo, msondo wa kizamani
Nikahusiwa upendo, upendo siri yake nini
Nimefundwa kimitindo, na starehe za chumbani
Kupendana ni matendo, mtendeane hisiani
Kweli mchezea jando, mapenzi kwake ni nini?
Bora niyapige tindo, mimi nawe buriani

No comments:
Post a Comment