Tuesday, May 16, 2017

Mr blue mboga Saba lyrics

Mboga saba umeniteka makahaba nawacheka
Kwenye mkataba nakuweka kwenye mahaba nakuweka
Napiga ibada usije lala kwenye mkeka
Aah kama vumba likikataa
Aah ndumba halitovaa
Bila nyumba chumba kimoja utakaa?
Nguo za mitumba nauliza mchumba utavaa? (Yeah)
Yeah basi mohoro nakupenda na ngozi yako nyororo
Kote unakwenda hata kwenye vigodoro
Penzi lako limenifunga minyororo
Basi leo twende wapi? Nichukue bajaji nije kwenu Masaki
Twende Coco Beach ukale mishikaki?
Au Zara Moon ukale ugali samaki?
Nachokupenda kuwa hujui kujivuna
Mtoto mzuri ila hujui kunichuna
Watoto wa uswazi hawajui kunikuna
Mapenzi kamari ila hujui kunipuna
Nilipiga goti kwa Mungu na dua ikafika
Haya maisha yangu na wewe ukaridhika
Eii…
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Unanifaa sana
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Nasikia raha
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Unanifaa sana
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Nasikia raha
Mtoto unajua njaa (mtoto) unajau raha
(Mtoto) kweli kifaa (mtoto) kweli unafaa
Moto bila ya mkaa ndoto ya kila star
We ni joto kwangu baridi balaa
Bonge la bambataa unapendeza unavovaa
Kwenye bed unavyocheza kama kwenye jukwaa
Macho ya kulegeza hii sio kungu nakataa
Kwenye giza waka waka kama taa
Ulaya bila visa nafika bila kupaa
Ah mama halali wa pendo
Achana na habari na skendo
Wanakaba kabari kila angle
Wanataka nife wateke mali wazibe pengo
Hawajui
Pengo langu halizibiki hawasumbui
Pendo gonjwa sugu halitibiki
Unapendwa na babu na bibi na mama na baba
Nakuita beki kwenye bonge la ligi unavyokaba
Mabrazameni ntawapiga shaba
Niacheni na mboga saba bakieni na makahaba
Nachompenda kuwa hajui kujivuna
Mtoto mzuri ila hujui kunichuna
Watoto wa uswazi hawajui kunikuna
Mapenzi kamari ila hujui kunipuna
Nilipiga goti kwa Mungu na dua ikafika
Haya maisha yangu na wewe ukaridhika
Eii…
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Unanifaa sana
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Nasikia raha
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Unanifaa sana
(Oh yee ye oyee oh yee ye oyee)
Nasikia raha
Oh yee ye oyee oh yee yee oyee
Oh yee ye oyee oh yee yee oyeeye

No comments:

Post a Comment