Tuesday, May 16, 2017

Mwana fa ft alikiba kiboko yangu lyrics

Kwa sifa moja umenikamata
Nakupa, we peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
Kila shetani ana mbuyu wake, we ni mibuyu mitatu
Ukiamua unitumikishe mwenzio ntalala na viatu
Najionea maajabu, najionea mapya mama angu
Hakuna mapenzi ya hivi popote kwenye ulimwengu
Siwezi elezea jinsi navyokuzimia
Nikicheza na moyo wako, unacheza na wangu pia
Nafsi yangu ilishapotea, siwezi hata kujitetea
Ka ulitoroka peponi uzuri ulivyokuenea
Piga la kushoto ntageuza na la kulia
Wengine hawanijaribu wanajua kitakachotokea
Sitaki mambo yaende kombo na yakienda yawahi kurudi
Hatuendi nayo, hatuwezi shindwa, yaje na mapambio ikibidi
Tunapishana, hatugombani then we back here
Hatuendi juu, hatuendi chini, love, we right here (oh!)
Hata mapenzi yakifa boo, si tubaki sawa tu
Si ni watu wazima, love hatuwezi kuishi ka underground
Ujue una nusu ya moyo wangu, na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe, una jua langu, una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu, we ndo Michelle Obama wangu
Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwanza
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu
Wakikuita vikao vya hino wambie uko busy na bwana
Na ubize hauwezi kuisha maana una mengi ya kufanya
Hatuwezi kosa usingizi sababu watu wanasema
Wana midomo, waifanyie nini? Waache wakichoka wataizima
Uko mikono salama, ’cause nakuzimia sana
Ka mboni yangu ya jicho jinsi navyokutazama
Mahaba to the moon and back
Kau keep it real, kwa kifupi mambo ya kihuni sitaki
Nataka tuzeeke pamoja
Mpaka vikongwe mi na we bega kwa bega
Chochote unachotaka nime mipango ya kukupa kweli
Kama sina ntatafuta na naamini utasubiri
Huwezi omba ndege una akili, huwezi omba meli
We ndo mtunza hela zangu, utaomba unachoweza himili
Ka mteka meli wa kisomali, we ndo captain wangu
We ndo suka man, we ndo pilot love
Ujue una nusu ya moyo wangu, na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe, una jua langu, una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu, we ndo Michelle Obama wangu
Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwamba
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu

No comments:

Post a Comment