Tuesday, May 16, 2017

Alikiba mac muga lyrics

LYRICS Verse 1 Ni mcheza bongo Mac Muga Yuko single sana Mac Muga Ukimwona kutwa kajinamia kwa sababu ya maisha yanamchanganya Long time ago alizamia Nakwenda kusini mwa Africa Huku pia alitanua kwa sababu ya maisha aliyofuma Alikuwa maarufu sana, Akajiona yeye ndo winner Full kujichanganya na wasichana Club zote za huko kujulikana Wewe Mac Muga Wewe wewe Mac Muga Ah, hii dunia, Mac Muga huruma! Chorus 2x Mungu si Athumani alipofika South Africa alikuwa na maisha bomba Ya juu, ya thamani tena yanayohitajika magari na kubwa nyumba x2 Ona sasa amesharejea, hajui wapi ataanzia! Hakuna kazi kutwa kajinamia Mac Muga hii ni dunia Maisha alichezea, gari ya kutembelea Shida walimwelezea wasichana na shida zao akawatatulia Hivi upewe nini Mac Muga? Mungu akupe nini Mac Muga? Nyumba ulijijengea, full kutanua Wewe ndio wewe, wengine fala! Wewe, Mac Muga Ona sasa umeshatibua! South Africa wamekutimua Na sasa home usharejea Wewe Mac Muga Mungu akupe nini Mac Muga? aah hii dunia, Mac Muga huruma Chorus 2x Mungu si athumani alipofika South Africa alikuwa na maisha bomba Ya juu, ya thamani tena yanayohitajika magari na kubwa nyumba x2 Ona sasa amesharejea, hajui wapi ataanzia Hakuna kazi ila akajinamia Mac Muga hii ni dunia! Verse 3 Yikes kama huoni kwa Mac Muga Huoni noma huruma kanyongonyea Afanye nini sasa, cha kufanya Kila anachachofanya anaona anakosea Yikes, kama huoni kwa Mac Muga Woi noma huruma kanyongonyea Afanye nini sasa, cha kufanya Kila anachachofanya anaona anakosea Akiwa jambazi gerezani ataishia Akiwa mwizi anaona atauliwa Akifikiria kujiua Nafsi inamsuta basi analia Wewe Mac Muga! Mungu akupe nini Mac Muga? oo dunia Mac Muga noma

No comments:

Post a Comment