Tuesday, February 27, 2018

Upo Hapo MwanaFA na AY - Fid Q

Everybody
B-Hits
B-Hits
B-Hits

Mipango baba
Baba sihitaji shida za waana mipango ya namba
Mipango baba
Baba sihitaji shida za waana mipango ya namba
Nanukia vizuri kama duka la perfume
Usiniite muhuni huwezi pata harufu ya ndumu
Hata beat sio kubumkubam ya kibishoo
Ila wana bado wakavu bishoo usilete hizoo
Najua kona zote kama ufagio wa zamani
Vichaka na chocho zote macho tu bila ramani
Ni kudra na mwanadamu nazi haishindani na jiwe
Lilopangwa liwe
Buggy jeans swag sio ya miaka 17 we baba
(Mzee baba)
Unataka vita na Mafia
Dili za mabilioni na bado tai huzioni
Winning togetherwanangu begani
Utanipenda bob wananiitaga mastermind
Mipango kwangu inachipua haina end
Uncle FA FAscobar usilete uchimvi
Navua gloves ila bado naupenda ugomvi

Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo

Hell Yeah kwa beat ya Hermy B
Fareed FA AY salu-te
Mzuka umefufuka toka enzi za ECT
Kikosi mstari wa mbele na nyuma haturudi
Uhkaa mkao wa kula kama ulivuna
Pambana na hili shangwe lisije likakutafuna
Tamani vyote ila chagua vya kumung’unya
Damn
Make sure mfuko umetuna
Kwenye giza mkononi mie nina tochi
Kuna vikosi mikosi gozi gozi
Kamata wa pembeni yako upige bao
Fanya yako usione hatari kama kuna wanga kibao
Na MasterCard mfukoni
Nimenyuka pamba kimtoni
Na sura ngumu kama stone
Ukijichanga tu hauponi
Biashara asubuhi mpaka asubuhi so jipange tu hommie
Muchiri waambie aterere ndio nini
Vibe liko juu kwanza mkeka haujachanika leo
Tank liko full leo masinema si video
El-Chapo bado nipo nipo
So nanyatia chipo chipo nisitoke draw UPO

Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo

Mie ndio yule mjamaa anayejua hadi anaboa
Kilichofanya nikakua sio raha ya ndoa
Ni kuzitua tamaa na njaa kuitoa
Ninapoamua kukamua mnajua inakaa poa
Niko tight kama Chabunene ndani ya skinny jeans
Hautaki kuja kati
Moonwalk kama Billie Jean
Wazee dili ni nini
Aisee mna akili nyinyi
Mie nina siri ya mjini na ya utajiri amini
Nnajua mie ninajitambua kitambo
Nawanywesha uhalisia ili muucheue ule ukweli wa mambo
Sitaki huko mbele ibaki misele au majuto au milupo kuwa tele
Yabaki madusko mfuko wa mafao
Kuna maisha baada ya groupie love
Sio kuti kavu mashuti nyavu
Mamluki hamnikuti bado mpo down

Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo
Upo hapo

Mipango baba
Baba sihitaji shida za wana mipango ya namba

No comments:

Post a Comment