Siku nyingi binti namfukuzia
Alishan’tosa nishakata tamaa
Sikujua kama kwangu angekuja
Nilitoa matumaini ya kumpata
Siku nyingi binti namfukuzia
Alishan’tosa nishakata tamaa
Sikujua kama kwangu angekuja
Nilitoa matumaini ya kumpata
(Leo hii kaja mwenyewe mchumba)
Ghetto kwangu mpaka ndani kaingia
(Nilimuuliza naeza kukusaidia)
Akacheka kisha akaniambia
Ombi langu lile amenikubalia
Siku zote alikuwa akinifikiria
Niliruka kwa furaha kubwa sana
Sikuamini kama mchumba ningempata
(Usilojua ni usiku wa giza)
Ningetambua bora ningemtimua
(Usilojua ni usiku wa giza)
Ningetambua bora ningemtimua
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
Baada ya stori binti nilimuuliza
Kinywaji gani angeweza kutumia
Alinieleza kisha mi nikainuka
Nikaelekea dukani kununua
Baada ya stori binti nilimuuliza
Kinywaji gani angeweza kutumia
Alinieleza kisha mi nikainuka
Nikaelekea dukani kununua
(Huwezi amini nyuma nilipomuacha)
Baada ya kurudi ndipo kizaa zaa
(Binti alikuwa kitandani kajilaza)
Nilimuamsha lakini hakuamka
Pumzi zake zilikuwa zimekata
Nilidhani labda kazimia
Maji ya baridi kichwani nilimwagia
Lakini hata hakushtuka
(Kumbe alikuwa tayari ameshakufa)
Nimekwisha Hussein bila kujua
(Kumbe alikuwa tayari ameshakufa)
Nimekwisha Machozi bila kujua
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
Ee Mola nimekosa nini
Ee Mola niokoe mimi
Ee Mola basi nipe akili
Mimi nifanye nini
Ee Mola nimekosa nini
Ee Mola niokoe mimi
Ee Mola basi nipe akili
Mimi nifanye nini
Furaha yangu imekuwa kilio changu (kilio changu)
Furaha yangu imekuwa kilio changu
Ndoto zangu leo majonzi kwangu
Ntawaeleza nini walimwengu
Ndoto zangu leo majonzi kwangu
Ntawaeleza nini walimwengu
(Vipi wataniona mi ni mkweli)
(Vipi nikiwaelezea wataniamini)
(Vipi wataniona sio katili)
(Vipi ingekuwa wewe ungefanya nini)
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
Nani ataniona mi ni mkweli
Nani nikimuelezea ataniamini
Nani ataniona sio katili
Nani atanisaidia mimi
12149191
ReplyDelete