Friday, December 30, 2016

Bob Junior Nichumu LYRIC

[Intro]
Oooh ooooh ooh
Ni Mr Chocolate
Bob Chocolate
Tuimbe wote, chocolate, chocolate
[Verse 1]
Kufuri imewekwa ili watu waseme
Basi acha mi nikwambie
Umekuwa dokta wa kuniponya
Basi acha mi nikusifie
Nishakuwa zoba, nikawa rofa
Basi acha kwako nitulie
Nilishaanguka ukaniokota, mzigo wangu usiachie
[Bridge]
Usijebadilika, ukawa kama wale
Wa enzi zile, zile, zile
Ukanitapika, ukawa kama wale
Wa enzi zile, zile, zile
[Chorus]
Sukari yangu, asali yangu
Mapigo yangu ya moyo wangu
Sukari yangu, asali yangu
Mapigo yangu ya moyo wangu
Basi nichumu nikiss mwaah
Nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah
Ahaa nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Ooh ooo
Ah raisi wa masharobaro nimechoka mimi aah
Ooh oooh ooo
[Verse 2]
Usimiss hadithi ya sungura na fisi
Acha ukweli nikwambie
Umenidhibiti, sihadaiki
Acha sifa nikupatie
Kula nanasi kwa hitaji nafasi
Basi acha nijiservie
Anaekushika mshikilie, shika basi usiachie
[Bridge]
Usijebadilika, ukawa kama wale
Wa enzi zile, zile, zile
Ukanitapika, ukawa kama wale
Wa enzi zile, zile, zile
[Chorus]
Sukari yangu, asali yangu
Mapigo yangu ya moyo wangu
Sukari yangu, asali yangu
Mapigo yangu ya moyo wangu
Basi nichumu nikiss mwaah
Nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah
Aah nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah
Aah nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah
Aah nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
[Outro]
Nichumu nikiss mwaah
Nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah
Aah nichumu nikiss mwaah
Basi nichumu nikiss mwaah, mwaah, mwaah
Masharobaro ndo habari ya mjini!

Bonge la Nyau ft Q Chillah Aza LYRICS

[Chorus – Q Chillah & (Bonge La Nyau)]
Aza, Aza, mtoto wa Kariakoo
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Aza, Aza
(Ah mtoto wa Kariakoo, mtoto wa Kariakoo)
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Kwenu wananiita golo
Ukweli sio koro
Mapenzi ndivyo yalivyo
[Verse 1 – Bonge La Nyau]
Eyo flow nazi-fix so bad
Navyo-feel bad just like na-play card
More motivation, more money, more play
Visa na vituko unavyofanya siongei
Ngwair, kama Ngwair akakuita She-Got-A-Gwan
Pozi mpaka pozi za Blue ukiwa chumbani
Ulivyodeka dah, ndo unanipa burudani
Umenipa thamani kwa mwingine sitamani
Kama umezaliwa mi nisota
Mwanao hata mia naokota
Ukirudi kwangu ka naota
Unavyonitunuku naogopa
Mtaka nyingi ukosa na saba
Usipende madingi utakuja kuvaba
Tulia na mimi tuishi pamoja
Tukikosa leo kesho inakuja
[Chorus – Q Chillah & (Bonge La Nyau)]
Aza, Aza, mtoto wa Kariakoo
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Aza, Aza
(Ah mtoto wa Kariakoo, mtoto wa Kariakoo)
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Kwenu wananiita golo
Ukweli sio koro
Mapenzi ndivyo yalivyo
[Verse 2 – Bonge La Nyau]
Ile love nayotaka kwako naipata
Siwezi kusaka vingine kwenye vichaka
Unavyokata, mpaka nadata
Kama love ni uchafu, Kkoo zitupwe taka
Mungu akupe imani uzidi kunithamini
Na akulinde na shetani ufate miongozo ya dini
Atuweke vyema duniani mpaka tukienda chini
Kila siku furahani: shida, raha na mimi
Kama umezaliwa mi nisota
Wanaogharami unaokota
Ukirudi kwangu ka naota
Unavyonitunuku naogopa
Mtaka nyingi ukosa na saba
Usipende madingi utakuja kuvaba
Tulia na mimi tuishi pamoja
Tukikosa leo kesho inakuja
[Chorus – Q Chillah & (Bonge La Nyau)]
Aza, Aza, mtoto wa Kariakoo
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Aza, Aza
(Ah mtoto wa Kariakoo, mtoto wa Kariakoo)
Aza, Aza, ah, nakupa shikamoo
Kwenu wananiita golo
Ukweli sio koro
Mapenzi ndivyo yalivyo

BUSHOKE FT K-LYNN - NALIA KWA FURAHA. LYSRICS

[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 1 – K-Lynn]
Unaposogea karibu, unaponishika mkono
Unaponitazama machoni, nashindwa vumilia
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
Najiuliza ni kwanini, hatukujuana mapema
Nimeishi na wasojua mapenzi
Wasojua hata kunyenyekea
Nimeishi na wanaojua ku-force
Wasojua hata kubembeleza
Ninapokuwa na wewe, najiona ndio mwenyewe
Hata kama sina pesa, najiona tajiri
Hata kama sijala, najiona nimeshiba
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 2]
[K-Lynn]
Naomba Mungu atujalie, tufunge ndoa mi na wewe
Na watoto pia tuzae, wakuite baba na mi mama
Maisha yangu bila wewe, sawa na basi bila konda
Maisha yangu bila wewe, mbele sitosonga
[Bushoke]
Na bado, na bado, sijafika mwisho
Na bado, na bado, sijamaliza kitabu
Vumilia maisha yangu, utakula vya kwangu
Mimi si wale wanaojisifu kwa ngono
Mapenzi si maneno, mapenzi ni vitendo
Na bado, na bado, nimesema bado
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata

Chege -- Mwanayumba LYRICS

Oyaeeh
[Intro]
Oyaee (check it out!), oyaaee
It’s A Fish Crab
Oyaeeh (Chege!), Mwanayumba
Oyaeeh (It’s a Fish Crab presentation), oyaaee
Oyaee, Mwanayumba
[Chorus]
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
[Verse 1]
Ujumbe wangu ni mfupi tu
Nawaombeni ndugu na jamaa
Popote pale mlipo oo
Msikiapo Chege naimba wimbo huu
Nahangaika kumtafuta, kipenzi changu Mwanayumba aah
Popote pale mtapomuona mwambieni bado nampenda
Sijui kama yuko Kenya, sijui labda yuko Dar Es Salaam
Sijui kama yuko Kigoma, mwambieni bado nampenda
Najua bado ananipenda, na mimi bado nampenda aa
Sijui nani kamchanganya Mwanayumba hayupo tena nami
[Chorus]
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
[Verse 2]
Mwanayumba kwani uko wapi nikufate mrembo ooh
Kama uko kwa mama yako mdogo nikufate Mabibo ooh
Mwanayumba kamwe bila wewe sitoweza mpenzi
Nimefunzwa kupenda nisiache tuwe enzi na enzi iii
Sasa wapi ulipokwenda mpenzi umeniacha na majonzi
Sikuoni tena mbele usoni nakuota kwenye njozi
Usiku navuta shuka napapasa sikupati
Aahaa aa aaah aa aah
[Chorus]
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
[Bridge]
Mkimuona, mkimuona
Mkimuona mleteni
Mkimuona, mkimuona
Mkimuona mleteni
Mkimuona yule pale, mkimuona mleteni
Mkimuona yule pale, mkimuona mleteni
[Chorus]
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
Mkimuona Mwanayumba mwambieni bado nampenda
[Outro]
Ee iye iye mwambieni bado nampenda
Yee iye iye mwambieni bado nampenda
Ee iye iye mwambieni bado nampenda
Yee iye iye mwambieni bado nampenda
Oyaeeh, oyaee
Oyaeeh Mwanayumba
Oyaeeh (check it out!), oyaee
Oyaeeh Mwanayumba

Chid Benz ft Alikiba --- Hasira Za NINI LYRICS

[Chorus – Alikiba]
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
[Verse 1 – Chidi Benz]
Chakula hakiliki kama nsipokuona
Haipiti chai iliki au ndafu ilionona
Laazizi, waubani, mchumba
Mashaallah, Mola kweli aliumba
Huna kasoro umejazika
Ila mlani kama godoro, kiuno umekatika
Nabangaiza vibarua mchana, usiku
Japo nipate chochote nije tule ipite siku
Maneno ya waongo wanaharibu makusudi
Usafiri mjini tabu napochelewa kurudi
Usinihisi vibaya ukanuna, ukavimba
Ukatamani unirarue, ugeuke simba
(Ugeuke simba baby, hasira za nini?
Hasira za nini, baby?)
[Chorus – Alikiba]
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
[Chorus – Alikiba]
Mami punguza hasira na unisikilize mimi
Please acha kuzira hivyo unaniumiza mimi
Sina mwingine zaidi yako haki ya nani
Moyo wangu uko kwako kwingine sitotamani
Nlizunguka pande zote, nkaona warembo wote
Kote nlisimama kwako naanguka niokote
Unanipa morali ya kutafuta mapesa
Najaza kibubu maisha mbele yasije tutesa
Pesa ndo kila kitu nazisaka mchana, usiku
Sipendi kushikwa karaha, nakwambia kila siku
Kokote kambi, chochote pwani, ndo life honey
Staki tuje lia njaa nazisaka nje, ndani
Jasho langu ili upate isikukumbe tamaa
Japo nilete mkate wakinishinda dagaa
Nipende usiniache mami, usije tambaa
Napokumbata nikumbate wangu wa shida na raha
Hasira za nini mamaa?
La Familia! Chidi Benz hapa
[Chorus – Alikiba]
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
Hasira za nini?
Kwanini huniamini
Kama mwenzio bado nakupenda?
Maneno mengi mjini, ili uniache mimi
Lakini mwenzio bado nakupenda
[Outro – Chidi Benz & (Alikiba)]
Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu
(Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu)
Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu
(Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu)
Mami usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Maendeleo kwa watu
Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu
Wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu

Christian Bella Ft Ommy Dimpoz Nani Kama Mama LYRICS

[Intro – Ommy Dimpoz]
Mama oh mama
Na Poz Kwa Poz!
Mama oh mama
Nani kama mama
[Verse 1 – Christian Bella]
Oh yah nani kama mama, heshima kwa mama
Yale mateso ulinibeba miezi mitisa tumboni mwako
Pole sana mama
Nikupe nini? Heshima kwa mamaaa (maama ee)
Uliteseka siku ya kunitoa duniani
Nikupe nini? (mama eeh)
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa
[Chorus – Christian Bella]
Mama ee
Nani kama mama aaa? (mama mama)
Nani kama mama aaa? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama aaa? (usipotoke umdharau mama yoyo)
Nani kama mama aaa? (ma ma ma mama)
[Verse 2 – Ommy Dimpoz]
Hello mama, hii ni kwako mama
Si, nimekukumbuka sana (mama)
Usiku na mchana, ai
Nakuombea upumzike salama eh
Tabia na heshima eh, busara na hekima eh ae
Ulinifundisha vyema eh, si, nakuombea upumzike salama
[Bridge – Ommy Dimpoz]
Matatizo ya dunia, kweli ninayapitia
Yale ulionihusia eeh, ya kweli mama ee
Matatizo ya dunia, kweli ninayapitia
Yale ulionihusia eeh, eee mama eeh
[Verse 3 – Christian Bella]
Malezi ya mama, elimu ya mama
Haina ada wala cheti ila ni zaidi ya elimu ya chuo kikuu
Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikilia usiku mama lazima utakesha na mimi
Huwezi kukubali niwe macho usiku
Nawe ufumba macho yako
Mapenzi ya maaama kwa mtoto wake haina mfano
Hata mapenzi ya boyfriend na girlfriend hayafiki hata robo
Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikiumwa usiku mama lazima utakesha na mimi
Mola wasaidie wakina mama wote
Wape maisha marefu, nani kama maama?
Mama ni maama yeeye
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa
Mama maama yeee, mama na mama
Nasema mama ni mama yee
Nani kama mama? (mama)
Mama ni mama (mama)
Heshima kwa mama
Mama ni mama
Wee!
[Chorus – Christian Bella]
Ma ma!
Nani kama mama aaa? (mama mama)
Nani kama mama aaa? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama aaa? (usipotoke umdharau mama yoyo)
Nani kama mama aaa? (ma ma ma mama)

Fid Q Propaganda LYRIC

[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda
[Verse 1]
Machungu unapozimwa, ili ufunikwe na asiyeweza
Mbaya zaidi wanampa promo lakini kwenye shoo nammeza
Hautaki kuwa tatizo sababu unaeza tatuka
Huwezi kujua wapi ntatua ka jiwe gizani likitupwa
Wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua
Hamkomi, igeni nione jinsi msamba mnaupasua
Hivi unaishi ili ule, au unakula ili uishi
Kumbuka a small lake will sink a ship
Mazingira hatarishi, mabwana afya wana pesa mob
Uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo
Ogopa kuoa haraka kama unaogopa taraka
Na uki-vote in a hurry jua una produce corruption
Maneno yao matamu, midomo yao inanuka
Ukipewa usisahau, ukitoa toa bila kukumbuka
Usiohofie kupitwa ili mradi muda haukuachi
Amini kesho itafika kama ipo ili uipate
Tunachukiana kwa sababu tunaogopana
Tunaogopana kwa sababu hatujajuana
Hatujuani kwa sababu tunatengana
Dunia ni nzuri walimwengu hawana maana
[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda
[Verse 2]
Polisi huniita mzurulaji na wanajua mi ni emcee
Kisha hunipa ishara ka wanavuta radi kwa tasdii
Baya lisilonizuru ni jema lisilo na faida
Nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha
Kuanzia kata, tarafa, wilaya, mikoa hadi ngazi ya taifa
Nikifa siachi skendo, na uhakika ntaacha pengo
Hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu
Pia ni kama live direction, struggle machoni mwa Chegu
Ukiwa mkali ka Marco Chali, raia wata-feel tu
Wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu
Urafiki sio urafiki usipochanganywa na kazi
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi
Hupaswi kumuamini muongo hata kama ataongea ukweli
Dhambi kutumia dini kama njia ya kutapeli
Wanajiingizia kipato kwa kivuli cha misaada
Hawatufunzi tuwe viongozi, labda viongozi wa kuwafata
Utata huja tunapoanza kuwachunguza
Badala ya kuwafuata ndipo siri zinapovuja
Tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga
Ukishindwa kujiendeshe ujue mwenyewe tu ulipenda
Kama umevutiwa na asali jiandae kumkwepa nyuki
Hauwezi kumtisha kwa mawe adui aliyeshika bunduki
Ni uchunguzi wa kisayansi ambao haukufanikiwa
Kama ng’ombe kula nyasi tu halafu akatoa maziwa
[Hook]
Polisi wana-support gangsta-rap ili uhalifu uongezeke
Wabana pua kuimba mapenzi, je itafanya ukimwi usepe?
Media zina-promote beef, wanadai zinakuza mziki
Wadau wana wasanii wabovu, nyie wakali mtatoka vipi?
Hizi ni propaganda, usiulize ni nani, ni yupi
Saa ngapi, ilikuwaje, na nani, ili iweje?
Hizi ni propaganda, utaibiwa ukicheza blunder
Yule last king wa Scotland sio Idd Amin wa Uganda