Saturday, December 24, 2016

MwanaFA ft. Dully Sykes & AY - Ameen

Intro:
Ni MwanaFA
Yupo na Dully Sykes
Silent Ocean
Inna Mi Yard
Keeping The Good Music Alive
Yessayah

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 1: MwanaFA
Ziende,on and on kama Eryka Badu/wafahamu sababu/ni heshima kwa Mungu/
Natembea kifua mbele yote sababu ya wewe/wote wanaojipindua mwisho wanasanda wenyewe/
Binamu yangu Masumbuko ananisikia hata akiwa jela/jinsi nakinukisha na bado juhudi na sala/
Naomba hekima za Suleiman/sio miguvu ya bure/hata kauli zangu ndogo zionyeshe nilienda shule/
Maadui wafunge mikono nimewazidi wape ishara/wape akili za hasara wachezee kazi na mshahara/
Ikidunda sana inakaribia kupasuka/yangu ikeshe isiishe leo hata wajukuu wanaikuta/
Bora kuchekwa kuliko kuchekwa sana wanaonipinga waumize,Mungu nakomba sana/
Uwape umri mrefu wa kwangu na wa babu yangu/ili roho zao ziumie wakiona mabalaa yangu/Amen..

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 2: MwanaFA
Nisichokijua hakiwezi kunisumbua/wakisema mabaya yashindwe kunifikia/
Wape kismati cha paka cha kupendwa na wachawi/mi naomba cha pesa na kwa ujinga niwe kiziwi/
Wape wanawake wazee na mafukara halafu wagonjwa/ama mabwana mabwabwa wasiogonga kabla ya kugongwa/
Wanaomba nisiwe na kitu ili niombe waninyanyase/dhiki inijae vyote vya kwangu wavipate/
Kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe/kama wanichukue msukule nisionekane wabaki wenyewe/
Naishi kwa kudra,baraka,matakwa yako/siwezi nikachemsha kama ukibaki upande nilipo/
Competition is irrelevant/with you by my side/nafanya siongei na wanajua mi ni mastermind/
Haraka zaidi yao/uchungu zaidi yao/ukubwa au udogo wa tatizo unaletwa na akili zao/it's a wrap

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee

Bridge:
Mi nna haraka zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/

No comments:

Post a Comment