Saturday, December 24, 2016

Fid Q ft. Yvonne Mwale - Sihitaji Marafiki





Verse 1.

Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani/
Udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani X2/
Haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao,
Washkaji ambao kosa lako lao wakati hauna mafao/
Wanaokufikiria wewe muda ambao/
Wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao/
Now
Kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi/
Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi Sihitaji urafiki na usupastaa/ukihit ndo unang'aa
Upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../
Kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground/
Sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau/
Wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
Ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza/
U-N-I-T na Prof. Ludi walionifunza kukaza
Kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea


Verse 2;

Na usupastaa huwa ni feki... utakung'arisha ukiwa na Market/
Utakupatia senti,utapita juu ya red carpet/
Utageuka young & restless, utakupa wanawake/
Utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake/
Kwahiyo power is not permanent.. huwa ipo kwa muda tu/
Respect your own conglomorete... fikiri kikubwa tu/
Masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu
Walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru/
Wanazusha najiskia.. so im my own best friend/
Sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/
Naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship/
Tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/
Na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea


VERSE 3

Rafiki wa kweli yukoje... ni mkimya au anayechonga/
Yule aliyekupa jina?au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?/
Au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ Hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/
Bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe/
Ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?/
Kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo/
Inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/
Unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/
Urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo/
Nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature/
Wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

2 comments: