Thursday, May 26, 2016

marlaw pii pii

[Verse 1]
Ninataka niwahi kufika
Njia inajam sasa wapi nitapita
Nimekaa karibia saa sita
Sasa kukaa nimechoka oh baby
Sijamwona long time now
Nimerudi toka mwezi jana
Nimeshakwambia mama nimefika tangu mchana
Anajua nimeshafika, ameshapika, amekasirika
Alipika tangu mchana, ila sasa lunch imegeuka dinner
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Bridge]
Ah ah, kuna jam baby
Ah ahh, hello
Ah ahh, hello
Ah ahh, hello
[Verse 2]
Unanikatia simu unanionea
Wewe ungekuwepo ungejionea
Unafanya hivyo unakosea mamaa
Unanikatia simu unanionea
Wewe ungekuwepo ungejionea
Unafanya hivyo unakosea mamaa
Nakuomba mpenzi ungojee
Ni njiani naja niombee
Nimechoka nakuja tule, huruma nionee
Nakuomba mpenzi ungojee
Ni njiani naja niombee
Nimechoka nakuja tule, huruma nionee
[Bridge 2] x2
Nimechoka kungoja highway
Nitapita popote imradi wee
Ili kama ni kesi na iwe (pii pii, hatuelewani)
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Bridge 1]
Ah ah (oh), I love you so much
Ah ahh, I love you mama
Ah ah, I love you mamaa
[Bridge 2] x2
Nimechoka kungoja highway
Nitapita popote imradi wee
Ili kama ni kesi na iwe (pii pii, hatuelewani)
[Chorus]
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Nimechoka kupiga honi now (pii pii), hatuelewani
Pii pii! Move out of the way, nimechoka kupoteza time
Nina siku nyingi kwenda home, I am missing my baby
Pii pii! Hello baby, natamani niwe nyumbani
Nimekwama hapa njiani, kuna jam baby
[Outro]
I love you so much, I love you Mama
I love you mama
I love you so much, I love you Mama
I love you mama
My baby, my baby
My baby, my baby
My baby, my baby

marlaw bembeleza

[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui bembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
[Verse 1]
Kila time nakuangalia usoni ma
Sio kamaa nakosa neno kusema
Ulivyo ma anafanya kosa kunena
Ingawa moyo hautaki kunena tena
Wazo kichwani lina beep (kukueleza)
Ilavibaya ukinijibu (bembeleza)
Nahisi sijui bembeleza
Utakataa halafu mi utaniumizaa
Kidesign nakuangalia usoni ma
Kuna sign za kuita huko machoni ma
Kitu fulani umehifadhi huko moyoni ma
Unachotaka nianze mikusema
Hapa unafanya nijione (nitashinda)
Hapa unafanya nitamke (nakupenda)
Ilaunacho jibu mdomoni nitofauti nausemacho machoni
[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
Hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
[Verse 2]
Kati yetu imetawala rangi ya pinki
Kitu ambacho moyoni siridhikii
Nacho kuomba tuwe zaidi ya marafiki
Inajionyesha machoni unaafiki
Lugha ya macho kwa sasa (nakataa)
Tataka tuongee ilitufikie (mwafaka)
Kwenye party ulikuja umependeza
Kwenye traini ukaniomba mi kucheza
Tuka-dance na macho umelegeza
Ulinibamba nikaficha kukueleza
Unanimaliza, mimi ninakweleza, ninakubembeleza
Baby please baby girl
Vile unatamka, wewe kuona nataka, tuonge ana kwa ana,
Baby please baby girl
[Bridge]
We Dada mi unaniumiza
We dada sijamaliza
Unakata simu
Please, usikate ma
[Chorus]
Hey hey hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza
Hallo ma
Laiti ungekuwa unaniona
Vile kila time nakonda nawaza
Kama kukupata nitaweza
Jinsi gani kukueleza
Au mi sijui kubembeleza
Usinikatae utaniumiza
Nakupenda kukutenda sitoweza

marlaw rita

[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
[Verse 1]
Rita we unajua jinsi gani mimi na wewe tulivyopendana
Jitoa sadaka kimapenzi ili mradi tusijetengana
Ila we unajua ni yako familia
Damu yangu ya Bongo si ya Asia
Ndo kigezo cha wao kunitosa
Mara mbili risasi wamenikosa
Kumbuka ile mimba ndio iliyokufanya ukaja kwangu (ulifukuzwa kwenu)
Ulijifunguapo mtoto na wote mkaishi kwangu (ukawachukiza kwenu)
Na taarifa ikaja kwako wewe Rita
Uende Arusha nduguzo wanakwita
Ukani-kiss kiss mimi na mtoto,
Nikaku-kiss ee eehee
[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
[Verse 2]
Ni tangu Arusha hadi Iringa simu inaita unapokea unalia
Kurudi Iringa uishi nami ndugu zako wamekuzuia
Ukasema laiti ungejua
Usingekubali uondokee pekee
Mwanao analia
Ona mumeo ni bora ninywe pombe
Ila kwa penzi uka-force kurudi
Piga simu mume wangu nakuja
Na maneno ya konda kwenye basi ulifika
Alikupa siti ukakaa, ulipokaa ukakaa
Ile siku mi nimelelewa
Niko mi na mwanangu, kumpokea mke wangu
Konda akasema si wewe, ila tu mwili wako
[Chorus]
Sauti inasikika
Tega makini, hujui nani inamwita
Chozi lanitoka
Nitazamapo angani, naona sura ya Rita
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kwamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
Ooh Rita Rita ahh
Na Marco Chali
Ndani ya MJ Records
This is true story to Marco
Rita, Rita, Rita
Aaah hata nyumbani kwangu haupo!

naona raha mbdogg

[Chorus]
Natamani nikuone, sijui ntakuona vipi
Natamani nikufuate, sijui ntakufuata vipi
Please baby I don’t know, sijui
Sema, sema, sema
Please baby I don’t know, sijui
Nakwagara sheri wange
[Verse 1]
Natamani mi nikupe moyo wangu
Uende nao
Uni-kiss niridhike moyo wangu
Upoe nao
Kama nilivyo, nipende mi msela
Mi msela aa, usiniache
Kukuacha naweza
Naogopa nitajiumiza
Ndo maana nafanya miujiza
Moyoni, usije niumiza
[Pre-Chorus]
Naona raha, naona
Raha, naona
Mwenzenu raha naona
Nahisi unafirigita
[Chorus]
Natamani nikuone, sijui ntakuona vipi
Natamani nikufuate, sijui ntakufuata vipi
Please baby I don’t know, sijui
Sema, sema, sema
Please baby I don’t know, sijui
Nakwagara sheri wange
[Verse 2]
Kipi mamaa, kinachokusumbua? Oh
Nieleze baby, ili nikupe mamii
Sema basi (basi), anaekuzuzua oh
Nieleze baby, nami nimuige muhuni
Nami najua, ni wewe tu ulie moyoni mwangu
Kwenye shida na raha, usinimwage
Usiniache
[Pre-Chorus]
Naona raha, naona
Raha, naona
Mwenzenu raha naona
Nahisi unafirigita
[Chorus]
Natamani nikuone, sijui ntakuona vipi
Natamani nikufuate, sijui ntakufuata vipi
Please baby I don’t know, sijui
Sema, sema, sema
Please baby I don’t know, sijui
Nakwagara sheri wange (wange)
[Bridge]
Dumba dumba, dumba dumbe
Dumba dumba, dumba dumbe
(Wange)
Dumba dumba, dumba dumbe
Dumba dumba, dumba dumbe
[Outro]
Ukitaka uje Afrika
Ukitaka twende Amerika
Ukitaka uje Afrika
Ukitaka twende Amerika
Ukitaka uje Afrika
Ukitaka twende Amerika
Ukitaka uje Afrika
Ukitaka twende Amerika
Ukitaka uje Afrika (Congo pia)
Ukitaka twende Amerika (Na Somalia)
Ukitaka uje Afrika (Nairobi pia)
Ukitaka twende Amerika (Kampala pia)
Ukitaka uje Afrika (Bujumbura)
Ukitaka twende Amerika (Comoro pia)
Ukitaka uje Afrika (Maputo aa)
Ukitaka twende Amerika
Dumba dumba, dumba dumbe
Nigeria
Dumba dumba, dumba dumbe
Hae hae hae
Dumba dumba, dumba dumbe
Hae hae hae
Hae hae hae

si uliniambia waja mb dogg

[Verse 1]
Si kwamba tu naimba sometimes huwa nalia
Hofu na mashaka ulipo labda una-share
Ulisema waja mnyamwezi nikakungojea
Sema mami sema lini utarejea?
Ee-eh eh, I love you maa
Oo-oh oh, I love you girl
Ee-eh eh, I love you maa
Oo-oh oh, I love you girl
Na uliposema waja wengi walikungojea
Mara muda umepita Abdul Bonge umeshamboa
Hivi kangoja mpaka Mola kamchukua
Sema mamii sema lini utarejea?
Ee-eh eh, I love you maa
Oo-oh oh, I love you girl
Ee-eh eh, I love you maa
Oo-oh oh, I love you girl
[Chorus]
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Ajabu toka ulipotoka miaka imepita
Sijakuona wangu my darling
Ni mbali uliko mi’ko mi na mashaka
Nakosa raha kabisa
[Verse 2]
Penzi lako nkilikosa baby kwangu soo
Ndo mana mi nakwita baby, baby kwangu njoo
Nakupa live baby unanitesa roho
Ndo maana nakonda, nadata na beat zapo
Au ndo ule mfano baby wanipenda roho
Na ile nyama mbichi baby, itaniuma roho
Kama ni dili ntazicheza baadae
Kwanza rudi home washangae
Rudi home baby ili wapagawe
Nicheze nawe Kuchi Kuchi Hota Haii
Nakusubiri baby, nakungojea mchumba
Nakusubiri nakungoja, mchumba usinizuge
Nakusubiri baby, nakungojea mchumba
[Chorus]
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Ajabu toka ulipotoka miaka imepita
Sijakuona wangu my darling
Ni mbali uliko mi’ko mi na mashaka
Nakosa raha kabisa
[Bridge]
Na kama waja niambie baby yee iye
Kama utanitosa mi nijua baby ei yee
Yaani na maana sina jinsi, I love you girl
I love you shori, everyday
Na maana sina jinsi, I love you girl
I love you shori, everyday
[Chorus]
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Si ulinambia kwamba waja
Man Dogg man, mi nakungoja
Ajabu toka ulipotoka miaka imepita
Sijakuona wangu my darling
Ni mbali uliko mi’ko mi na mashaka
Nakosa raha kabisa

mb dogg latifah ft madee

[Verse 1 – MB Dogg]
Maneno mengi wanasema juu yako
Eti kuna kitu honey umenifanyia
Mganga sio sababu mimi kuja kwako
Ila mi mwenyewe moyoni nimekuchagua
Nakutafuta, nione sura yako
Nakutamani, niwe karibu yako
Kama ni gari ndio mapenzi yawe tight
MB Dogg man, mi nishalinunua
Kama salamu honey we ukini-miss
Ni-beep baby, mi nitakupigia
Nakutafuta, nione sura yako
Nakutamani, niwe karibu yako
Aaya aa baby
Yei yei yei, oh baby
[Chorus – MB Dogg]
Sema basi unachotaka mamii
Sema basi unachotaka honey
Honey achana na mawazo kishetani
Ukiniacha mi nitabaki na nani?
Latifah we ndo tu mamii
Lati we ndo honey
Latifah we ndo tu mamii
Latifah, haya!
[Bridge – MB Dogg]
Yei yei yee, yee baby
Aah aa, oo oh
Yei yei yee, yee baby
Aah aa, oo oh
[Verse 2 – Madee]
Vipo vya ku-share Lati sio mapenzi
We ni wangu imepangwa toka enzi
Sema basi kitu gani unachotaka
We usijali mrume sina matata
Nachotaka we milele uwe wangu
Uje nikuite mama wa watoto wangu
Ukiniacha utaumiza moyo wangu
Kwani n’shaachana na habari za machangu
Ndio, sharo wacha waone donge (waone donge)
Kama mikwanja tutachota club tubonge
Kilichobaki sir God tumuombe
Tuwapo wawili nyoyo zetu tuzikonge
Nachotaka we milele uwe wangu
Uje nikuite mama wa watoto wangu
Ukiniacha utaumiza moyo wangu
Kwani n’shaachana na habari za machangu
[Verse 3 – MB Dogg]
Penzi la dhati Latifah mi nitaona ah
Haa aa haa a
Penzi la uzushi Lati mi nitajua ah
Haa aa haa a
Kumbuka Doggy man, Dogg nakupenda
Ukiniacha Doggy man, Dogg nitakonda
Njoo uni-kiss lady, njoo unipe denda ahaa
Madee ye anajua
Kama penzi langu kwako moyoni kidonda
Haa aa haa a
Kama penzi langu kwako nguvu za kiganga
Haa aa haa a
Ukiniacha Doggy man, Dogg nitakonda
Njoo uni-kiss lady, njoo unipe denda ahaa
Dogg naumia
[Bridge – MB Dogg]
Yei yei yee, yee baby
Aah aa, oo oh
Yei yei yee, yee baby
Aah aa, oo oh
[Chorus – MB Dogg]
Sema basi unachotaka mamii
Sema basi unachotaka honey
Honey achana na mawazo kishetani
Ukiniacha mi nitabaki na nani?
Latifah we ndo tu mamii
Lati we ndo honey
Latifah we ndo tu mamii
Latifah, haya!

Kiboko Yangu Ft. Alikiba

[Intro – Alikiba]
Kwa sifa moja umenikamata
Nakupa, we peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
[Verse 1 – MwanaFA]
Kila shetani ana mbuyu wake, we ni mibuyu mitatu
Ukiamua unitumikishe mwenzio ntalala na viatu
Najionea maajabu, najionea mapya mama angu
Hakuna mapenzi ya hivi popote kwenye ulimwengu
Siwezi elezea jinsi navyokuzimia
Nikicheza na moyo wako, unacheza na wangu pia
Nafsi yangu ilishapotea, siwezi hata kujitetea
Ka ulitoroka peponi uzuri ulivyokuenea
Piga la kushoto ntageuza na la kulia
Wengine hawanijaribu wanajua kitakachotokea
Sitaki mambo yaende kombo na yakienda yawahi kurudi
Hatuendi nayo, hatuwezi shindwa, yaje na mapambio ikibidi
Tunapishana, hatugombani then we back here
Hatuendi juu, hatuendi chini, love, we right here (oh!)
Hata mapenzi yakifa boo, si tubaki sawa tu
Si ni watu wazima, love hatuwezi kuishi ka underground
Ujue una nusu ya moyo wangu, na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe, una jua langu, una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu, we ndo Michelle Obama wangu
[Chorus – Alikiba]
Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwanza
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu
[Verse 2 – MwanaFA]
Wakikuita vikao vya hino wambie uko busy na bwana
Na ubize hauwezi kuisha maana una mengi ya kufanya
Hatuwezi kosa usingizi sababu watu wanasema
Wana midomo, waifanyie nini? Waache wakichoka wataizima
Uko mikono salama, ’cause nakuzimia sana
Ka mboni yangu ya jicho jinsi navyokutazama
Mahaba to the moon and back
Kau keep it real, kwa kifupi mambo ya kihuni sitaki
Nataka tuzeeke pamoja
Mpaka vikongwe mi na we bega kwa bega
Chochote unachotaka nime mipango ya kukupa kweli
Kama sina ntatafuta na naamini utasubiri
Huwezi omba ndege una akili, huwezi omba meli
We ndo mtunza hela zangu, utaomba unachoweza himili
Ka mteka meli wa kisomali, we ndo captain wangu
We ndo suka man, we ndo pilot love
Ujue una nusu ya moyo wangu, na nusu ilo baki kwangu
Yote nakupenda wewe, una jua langu, una mwezi wangu
Unatembea na roho yangu (wewe)
Sio mtu tena wa mademu, we ndo Michelle Obama wangu
[Chorus – Alikiba]
Kwa sifa moja umenikamata
We peke yako ndo umeniweza
Nilikopita nimeteleza
Lakini kwako, we ndo kiboko yangu
Sipagawi hawajui kwamba
We namba moja umewakimbiza
Unatembea na roho yangu
Nataka ujue we ndo kiboko yangu