Wednesday, August 31, 2016

Marlaw - Rita

oh rita rita
oh rita rita oh no no
sauti inasikika, tega umakini ujue nani inamuita
chozi lamtoka, nitazamapo angani naona sura ya rita
ona mikono yangu mitupu, hii mizuri ya kukushika mpenzi
hata nyumbani kwangu haupo, umepotea sikuoni mpenzi
oh rita oh rita, daily nakuwaza we
oh rita oh rita, mi nitanyamazaje?

ah
rita we unajua jinsi gani mi na wewe tulivyopendana
nimejitoa sadaka kimapenzi ili mradi tusije tengana
ila, we unajua ni yako familia,
damu yangu ya bongo si ya asia
ndo kigezo cha wao kunitosa
mara mbili hivi sasa umenikosa
kumbuka ile mimba ndo ilokufanya ukaja kwangu...ulifukuzwa kwenu!
ulijifungua poa mtoto na wote mkaishi kwangu... ukawachukiza kwenu!
na taarifa ikaja kwako wewe rita
uende arusha nduguzo wanakuita
ukani'kiss kiss mimi na mtoto
nikaku'kiss yeah!

sauti inasikika, tega umakini ujue nani inamuita
chozi lamtoka, nitazamapo angani naona sura ya rita, [sura ya rita]
ona mikono yangu mitupu, hii mizuri ya kukushika mpenzi
hata nyumbani kwangu haupo, umepotea sikuoni mpenzi
oh rita oh rita, daily nakuwaza we [rita we]
oh rita oh rita, mi nitanyamazaje?

ni tangu arusha hadi iringa simu inaita unapokea unalia
kurudi iringa uishi nami ndugu zako wako wamekuzuia
ukasema laiti ungejua, usingekubali uondoke peke
mwanao analia, ona mumeo ni bora ninywe pombe
ila kwa penzi uka'force kurudi piga simu mume wangu nakuja
na maneno ya konda kwenye basi ulifika
akakupa siti ukakaa, ulipokaa ukakaa
ile siku mi nimelewa niko mi na mwanangu kumpokea mke wangu
konda akasema si wewe, ila tu ni mwili wako

sauti inasikika, tega umakini ujue nani inamuita
chozi lamtoka, nitazamapo angani naona sura ya rita
ona mikono yangu mitupu, hii mizuri ya kukushika mpenzi
hata nyumbani kwangu haupo, umepotea sikuoni mpenzi
oh rita oh rita, daily nakuwaza we
oh rita oh rita, mi nitanyamazaje?

oh rita rita ah rita
ah eh
rita hata nyumbani kwangu haupo

No comments:

Post a Comment