la moyoni by Dogo Janja ft PNC
wala mimi sina hila, ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
wala sina kisasi, namshukuru mola huko nilikotoka na sasa nilipofika
kitanashati haswa, natiririsha ngoma
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
kitanashati haswa, nakinukisha pale
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
Verse zangu mi naziacha mungu atawasomea
Jasho langu kwenye shamba lao, walifanya Mbolea
Hawakujali nilikotokea, shida zajibebea
wakanifunga akili huku miguu inatembea
Mama akasema mwanangu kaza msuli
Ukitaka zikwa na watu vua koti la ukiburi
Dawa ya Jeuri kiburi, mimi sio mzuri
Pesa ndio kivuli nalea mapenzi kama hujui
kudai haki yangu kumejenga uadui
napenda 'madugu' zangu na ndugu siwabagui
mtanizika na simjui, ntapoelekea asubuhi
nani mwenye upendo wa ukweli hata nikishuka haupungui
Bado nasukuma kete, weka nami niweke
chomeka nichomeke ngumi dabo na teke
kwenye maseke ya makeke
mfukoni mambo bado kama Chege wa Temeke!
wala mimi sina hila, ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
wala sina kisasi, namshukuru mola huko nilikotoka na sasa nilipofika
kitanashati haswa, natiririsha ngoma
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
kitanashati haswa, nakinukisha pale
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
Naamua kukaa kimya, ila nina domo la kaya
Hata we niliyekuamini, leo unanisema vibaya
stoneshi kidonda binadamu ka' kinyonga
ukitaka kuishi wanavyotaka, he utakonda
wako waliofurahi, wakasema naenda kuteseka
kumbe kwangu bora maana hata nikilala kwenye mkeka
siwezi kukataa nimetoka kwenye njaa
kama hakuna manufaa siwezi ng'ang'ania Dar
Jasho nililomwaga halijachonga hata kitanda
watu wanaendesha magari na kumiliki vinanda
Inshallah, Mungu ndiye anayepanga
Machungu naya'rewind kwenye mind kama kanda
Nashukuru asubuhi kumekucha kwenye mwanga
Mungu ananilinda ananikinga na Majanga
Namuomba safari hii isiishie njiani
waje sema maisha yangu bila wao haiwezekani
wala mimi sina hila, ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
wala sina kisasi, namshukuru mola huko nilikotoka na sasa nilipofika
kitanashati haswa, natiririsha ngoma
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
kitanashati haswa, nakinukisha pale
shukrani pia ziende kwa Ustadhi Juma Musoma
Mziki kwenye ala, nawasukuma kama mpira
kama nafunga kushoto kumbe kulia..Bila!
Ndege mjanja tundu mlinzi tatu..Bila!
Janjaro bado yupo kama desturi na Mila
Right!
Niko makini, kwenye game sitong'oka
Japo kuna wanga wanaotaka kuzima nyota
kuna wanaodiriki, hata fala mi kuniita
ila mridi nipinde, wao wabaki wakipeta
ila nimeshtuka, siri ndo imefichuka
mwanzo walipoona fani na sasa wapo jukwaani
walo.sema ni uhuni watu imewaingia damuni
wengine bila haya