Thursday, December 6, 2018

subira by shaa

Intro:
Shika uliposhikwa,ujinga kuachia
Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia x2
Chorus:
Maneno x3
Hayashibishi mtu...
Maneno x3
Ila yagombanisha watu (repeats twice)
Verse 1
Hizi ni salamu,nakupatia Subira,nisipokuwepo nitakuwa nasikia
Hizi ni salamu nakupatia Subira mama,nisipokuwepo nitakuwa nasikia
Oooh Subira nisikize sana uendapo mbeleni kuna mawifi ujichunge sana
Oooh Subira nisikize sana uendapo mbeleni kuna mawifi ujichunge mama…
Acha kusangalai (Umpende mumeo)
Weh acha kusangalai (Umtunze mumeo)
Ogopa sanaaa (Kovu la ndui halifutiki)
Hayana maana (Maneno maneno ya wanafiki) X2
Chorus
Maneno x3
Hayashibishi mtu...
Maneno x3
Ila yagombanisha watu (repeats twice)
Verse 2
Mambo ya zamani tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani zitunze kifuani mwenzangu
Mambo ya zamani tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani zisiwafikie walimwenguuu
(Aaah chunga mdomo unajidanganya
unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya)
Shoga eh kumbuka wanaume sikuhizi wachache
Akienda bafuni akienda kazini akuage shoga eh
(Aaah chunga mdomo unajidanganya
unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya)
Aaaah hiyo nafasi usiipate uiache utachekwa weh
Wenzio wamaliza soli kwa waganga waipateee
(Aaah chunga mdomo unajidanganya
unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya)
Shaa (Hehehe, maji ya ugali hayaonjwi mwenzangu
eh..Wee mwana mwana mwanangu weeehhh...eeeehhh)
Utaniacha hoi hoi hoi,hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi hoi hoi,hata nikikuona sauti sitoi
Shoga eh kumbuka wanaume sikuhizi wachache
Akienda bafuni akienda kazini akuage shoga eh
(Aaah chunga mdomo unajidanganya
unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya)
Shaa(We Shirko weh jamani we Shirko wewe...
Shughuli imeambata na mvua hii
wanyama wanakula wima,chezeya...
Vita vifanyike ila Raisi nisiuwaweeee..)
(Aaah chunga mdomo unajidanganya
unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya)
.................
Utaniacha hoi hoi hoi,hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi hoi hoi,hata nikikuona sauti sitoi
..............piano plays till fade

No comments:

Post a Comment