Oi yeh
Olelele
Wasafi Records
Alfajiri imefika
Anga inang’aaa
Mvua inaanza katika
Ghafla tumbo la njaa
Naweka sauti kwa spika
Nipate umbea wa Dar
Mara simu inaita
Jina la Anko Twaha akisema
Mama yu hoi kitandani
Kama si wa leo wa kesho
Na kupona sidhani
Upate japo neno la mwisho
Mi ndo mtoto wa pekee
Nyumbani wananitegemea
Mdogo wangu wa kike
Hali duni alishagaolewa
Tazama jasho langu la mnyonge
Kipato hakikidhi mahitaji
Napiga moyo konde
Yarabi Mola ndo mpaji
Matatizo
Matatizo
Yatakwisha lini
Matatizo
Kila siku mimi (ewe Mola)
Matatizo
Yatakwisha lini
Japo likizo
Nifurahi na mimi
Mola aliniumba na subira
Imani pekee ngao yangu
Mbona nishasali sana
Ila mambo bado tafarani
Mama kanifunza kikabila
Ikunde sanda haimi yangu
Tena nijitume sana
Na vya watu nisivitamani
Hata mpenzi nilo nae
Najua siku atanikimbia
Itanitesa ye ndio nguzo
Zile ngoja kesho
Baadae atazichoka kuzivumilia
Anakosa hata matunzo
Ona
Nadaiwa kodi nilipopanga
Nashinda road nikiranda
Nishapinga hodi kwa waganga
Kwa kuhisi nalogwa
Nikauza maji na karanga
Nikawa dobi kwa viwanda
Ila kote ziro ni majanga
Mtindo mmoja
Mi ndo mtoto wa pekee
Nyumbani wananitegemea
Mdogo wangu wa kike
Hali duni alishagaolewa
Tazama jasho langu la mnyonge
Kipato hakikidhi mahitaji
Napiga moyo konde
Yarabi Mola ndo mpaji
Matatizo
Matatizo
Yatakwisha lini
Matatizo
Kila siku mimi (ewe Mola)
Matatizo
Yatakwisha lini
Japo likizo
Nifurahi na mimi
No comments:
Post a Comment