Nitafanya
Kidum
Lady Jaydee
Verse 1 (Kidum)
Ikiwa umeamua kunitoroka
ikiwa unahisi hujiskii nami tena
na mbona imekuwa ngumu kunidokeza
naona ni bora nilie leo, badala ya kesho
kupenda, usipende
ni kama kujitia kitanzi
nitachimba na sururu
kwa ardhi nikitafuta penzi lako
ni heri nipigwe fimbo kwa mwili
sababu ntajikuna ama ntajikanda na maji moto
maumivu ya penzi, mtu hajikuni
wala hajikandi na maji
na hakuna upasuaji
Chorus
kama
kuna kosa nimewahi fanya (nielezee)
kama
kuna jinsi tunaweza leta (mpaka niishi)
na kama
kuna kitendo linaweza tendwa (nielezee)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
Verse 2 (Lady Jay Dee)
kweli hukumbuki ulioyafanya
ni kweli unakumbuka tulikotoka
sisemi habari zozote za kusikia
bali kwa ushahidi niliouona
msamaha mara ngapi
umeshaomba na bado
chenye makosa mangapi
niliyoyafumbia macho
mpaka leo nahisi kufika kikomo
maumivu yanazidi
ndani ya moyo
sitaki kwenda mbali kwani uko moyoni
nikusamehe mimi mara ngapi wee
nielezee mpenzi mara ngapi
Chorus
unataka nikusamehe mara ngapi (usihesabu)
ungependa nikuvumilie mara ngapi (hii ni ya mwisho)
je wewe nikulilie mara ngapi (vumilia)
sitoweza (utaweza wee)
nimechoka (usichoke)
nimeshindwa (usishindwe)
naondoka (usiondoke)
sitoweza (utaweza yee)
nimechoka
nimeshindwa (usishindwe)
naondoka (usishindwe)
Verse 3
ukihesabu mara ngapi umenisamehe
ni kama kuhesabu
ni mara ngapi mtoto kaharibu nappy
usichoke
usiondoke
usilie
niko hapa kukulinda
Chorus
kama
kuna kosa nimewahi fanya (nielezee)
kama
kuna jinsi tunaweza leta (mpaka niishi)
na kama
kuna kitendo lingeweza tendwa (nielezee)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
nitafanya (fanya)
nitatenda (tenda)
unataka nikusamehe mara ngapi (usihesabu)
ungependa nikuvumilie mara ngapi (hii ni ya mwisho)
je wewe nikulilie mara ngapi (vumilia)
sitoweza (utaweza wee)
nimechoka (usichoke)
nimeshindwa (usishindwe)
naondoka (usiondoke)
sitoweza (utaweza yee)
nimechoka
nimeshindwa (usishindwe)
naondoka (usishindwe)
No comments:
Post a Comment