Kisiwa cha Malavidavi
ZAnto
Verse 1
Kwa kweli nilikuwa napenda sana
Mechi za nje za ujana
Aliyekuwa mke wangu
Analia aah
Kwa kweli nilikuwa napenda sana vibinti
nakuwahonga mpaka magari
Waliyekuwa watoto wangu
Wanateseka na njaa
Mitungi kila saa
Nyumbani sina time ya kukaa
Marafiki nami
Night club na mimi
Sasa nimebaki lonely
Track redioni hazichezwi
Yaani pesa hakuna, marafiki hakuna
Hata bebi hunitaki tena
Sasa nimebaki lonely
Track redioni hazichezwi
Yaani pesa hakuna, marafiki hakuna
Hata bebi hunitaki tena
Chorus
Nakupenda aiyaa
Nakupenda sana bebi
Nakuhitaji mama mama
Njoo kisiwa cha malavidavi
Nilikutenda aiyaa
Nisamehe my baby
Nakuhitaji mama mama
Njoo kisiwa cha malavidavi
Verse 2
Sielewi tena nisikize ma
Kwani najua pombe ndiyo chanzo ah
Kilichofanya nikutende dharau kibao
Ndani ya nyumba hakuna raha
Na kwangu ulikuwa dhaifu nisikize ma
Kwani najua kweli ulinipenda ah
Watoto wangu niliwatenga
Nisamehe mpenzi we unasema
Sitaki rudia tena
Najuta kwa yote niliyofanya
Nisamehe na goti napiga, nalia ahh
Sasa nimebaki lonely
Track redioni hazichezwi
Yaani pesa hakuna marafiki hakuna
Hata bebi hunitaki tena
Sasa nimebaki lonely
Track redioni hazichezwi
Yaani pesa hakuna marafiki hakuna
Hata bebi hunitaki tena
Chorus
Nakupenda aiyaa
Nakupenda sana bebi
Nakuhitaji mama mama
Njoo kisiwa cha malavidavi
Nilikutenda aiyaa
Nisamehe my baby
Nakuhitaji mama mama
Njoo kisiwa cha malavidavi
Uje kwenye kisiwa cha malavidavi
Uje tupeane mapenzi
Usisahau na wanangu
Sahau yaliyopita na tugange yajayo
No comments:
Post a Comment