Saturday, November 14, 2020

Gwiji mwana fa lyrics

 Ooh

Falsafa

Aah MwanaFA
Nkoyi
Omeki okangami
wewe ni gwiji wa magwiji
Asiyekubali aumbe dunia yake
Lakini mimi Nyoshi El Saadat
Nakuchukuliaga kama Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Zabanga
Le Martial Bosomba Seskuule hahahah
Never end never lose
MwanaFA
Légende
Légende
Légende

Naota ndoto hazina rangi naamka nazipaka
Watoto wa kiswazi huwezi ukatuwekea mipaka
Mungu ndio ametakajongoo kawa nyoka
Hakuna kiunzi hatuwezi ruka
Tushasukuma sana milango iliyoandikwa vuta (vuta)
Niamini na inafunguka
Mbwa mkali usikatize wahuni tunapita
Tunayavuka kwa kamba madaraja yaliyovunjika
Mungu wetu halali wala haendi likizo
Hatuachi kumuomba na anafuta matatizo
Yakija tena naomba tena na Mungu anayafuta tena
Mioyo yetu ipo safi safi ile kinoma
Kifo kiniue au maumivu yanikomaze
Yote sawa ila ujinga usinipumbaze
Kila kiumbe ana njaa yake moyo na tamaa zake
Mbwa mpumbavu ndio anaweza bwekea ndege

Waite wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite waite waje wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite waite waje wamuone gwiji wajigambe (we haya)

Mi ni hustler babe that’s what I do I hustle
Shida hazikwepeki zipo kukupima muscle
Zikutoe macho zikutoe jasho
Zikupe akili na zikuandae kwa kesho
Jikaze mwana usichukuliwe mateka
Ka unaachana na dunia we ndio uandike talaka
Ukiomba mafanikio fahamu yanakuja na wivu
Havitengani havikai mbali kidevu na ndevu
Dunia haitasimama ukigoma kutembea nayo
Sio magumu ka ku click link kwa bio
Kakamaa nakupa moyoumegusa tu button siyo
Kuwa mpambanaji kama binamu yangu Suyo
Huu sio mziki wa mafala ni mziki wa mataita
Unakuweka kitako na chaki unakufundisha
Una’feel the passion zaidi ya telemundo
Mapanchi mengi hata Touch akizima mdundo
Bye bye

Waite wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite waite waje wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite wamuone gwiji wajigambe (we haya)
Waite waite waje wamuone gwiji wajigambe (we haya)

Is another one
Touch (touch)

We haya
Uuh
We haya

No comments:

Post a Comment