Friday, February 10, 2017

kemosabe by Fid Q lyrics

Niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/
Sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/

Kwahivyo nikaenda Dar na treni... of thoughts../
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/

Sikutaka kuivaa mikosi..nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport..password.. pin..lakini ni crack codes/

Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/

Je mimi ni kaka mubaya...? kaka aso haya../
KAKA..? huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka.. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/

Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui?

Mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball.... hata kwa mpira wa makaratasi/

Unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/

Ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE.. life ni zaidi ya ku-have fun/

Kwani.. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/

Ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/

Nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/

Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/

Ndiyo.. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/

Mie ni mbishi.. muulize Nikki - hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba..

No comments:

Post a Comment