Sunday, July 31, 2016


HUU HAPA UTHIBITISHO.

Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza,

Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani ( SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, beats kali, management nzuri and all that, kitu gani kilimkimbiza SHAROBARO RECORDS?

Ona babio mamio wote wanakulilia,

HAPA ALIKIBA ANAMAANISHA, SHAROBARO RECORDS, WAKIONGOZWA NA BOB JUNIOR, WOTE WANAMLALAMIKIA DIAMOND KWA KITENDO CHAKE CHA KUKIMBIA KUFANYA KAZI SHAROBARO. (BOB JUNIOR ALIPIGA KELELE SANA DIAMOND ALIPOKIMBIA SHAROBARO RECORDS )

Mtoto pekee ako nyumbani, kipi kimekukimbiza,

HAPA ALIKIBA ANASEMA, DIAMOND ALIKUWA NDO ARTIST PEKEE MKALI ALIYEKUWA CHINI YA SHAROBARO RECORDS. HAKUKUWA NA UPINZANI WOWOTE NDANI YA SHAROBARO, KITU GANI KILIMFANYA AONDOKE ?

Ona babio mamio wote wanakulilia



Ndani ya Dar es salame ulikuja bure


HAPA ALIKIBA ANAMKUMBUSHA DIAMOND, KUWA SIKU ALIPOKWENDA SHAROBARO RECORDS KWA MARA YA KWANZA, HAKUWA NA HATA SENTI TANO NA ALIREKODIWA WIMBO WAKE BURE KABISA.NENO DAR ES SALAME, LIMETUMIKA KUMAANISHA SHAROBARO RECORDS AU MUSIC INDUSTRY.
(KAMA ULIKUKUWA HUJUI, ALIKIBA NI MMOJA KATI YA WANAHISA WA SHAROBARO RECORDS, NA NDIO ALITOA IDHINI KWA BOB JUNIOR, AREKODI BURE WIMBO WA DIAMOND. ILIKUWA HIVI DIAMOND ALIENDA KWA BOB JUNIOR NA KUMWAMBIA ANA WIMBO WAKE ANAOMBA UREKODIWE LAKINI HANA UWEZO WA KIFEDHA, BOB JUNIOR AKAOMBA KUMSIKILIZA, ALIPOMSIKILIZA AKAGUNDUA KIPAJI CHA DOGO, BUT HAKUWA NA MAMLAKA YA KUREKODI WIMBO HUO BURE BILA IDHINI YA BOSS, ALIKIBA, SO IKABIDI AENDE KWANZA KUOMBA IDHINI KWA ALIKIBA, ALIKIBA AKAMWAMBIA BOB JUNIOR KAMA DOGO ANAJUA KUIMBA VIZURI, MREKODIE TU, HAKUNA SHIDA. ALIKIBA ALIYASEMA HAYA AKIWA ANAYAFANYA MAHOJIANO KWENYE KIPINDI CHA MKASI HIVI KARIBUNI.

Tena kimwana, kimwana hujui kuchuna

WAKATI DIAMOND, ANAENDA KUOMBA KUREKODI KWA BOB JUNIOR, ALIKUWA TAYARI KUFANYA SHOW ZAKE HATA BURE ILIMRADI TU AWEZE KUJITANGAZA..DIAMOND ALIWAHI KUMUOMBA ALIKIBA, APANDE NAYE KWENYE SHOW YA ALIKIBA, BILA MALIPO YOYOTE ILI WATU WAMUONE AKIWA NA ALI KIBA. SO ALIKIBA AMETUMIA NENO "KIMWANA ASIYE JUA KUCHUNA" AKIMAANISHA 'MSANII UNDERGROUND ALIYE TAYARI KUIMBA HATA BILA MALIPO.



Na zile lawama za wale walokuzoeza,

HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA LAWAMA ZA MADEMU WANAO TOSWA NA DIAMOND


Ulikuja jana na leo tofauti sana.

HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEBADILIKA KITABIA BAADA YA KUPATA MAFANIKIO KIMUZIKI.


Tena bora Yule wa jana, wa leo tofauti sana,

HAPA ALIKIBA ANAWAZUNGUMZIA WEMA SEPETU NA PENNY, ANASEMA BORA HATA PENNY KULIKO WEMA AMBAYE NDIO YUPO NA DIAMOND KWA SASA

Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma

HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA TABIA TABIA ZA WEMA SEPETU. MKOROFI(DAKIKA MBILI MBELE NYUMA), NA MWINGI WA HABARI, AMA PASUA KICHWA ( KICHWA KINAUMA) AMA KICHECHE.


Tena bora Yule wa jana, wa jana leo wa jana,

HAPA ALIKIBA ANASISITIZA ANACHO KIMAANISHA, KWAMBA ANAMZUNGUMZIA WEMA, " tena bora yule wa jana, wa jana leo wa jana " YANI YULE AMBAYE UPO NAE LEO, NA AMBAYE ULIWAHI KUWA NAE ZAMANI. NI WA JANA, UPO NAE LEO, LAKINI ULIWAHI KUWA NAYE JANA. HUYO NI WEMA SEPETU, ALIWAHI KUWA NA DIAMOND, WAKAACHANA, WAMERUDIANA TENA. ( 'WAJANA LEO WA JANA = WEMA SEPETU )


Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma
HAPA ALIKIBA ANAKUTOLEA UFAFANUZI ZAIDI KWAMBA, HUYU " WA JANA LEO WA JANA" SI MWINGINE ILA NI WEMA SEPETU. ANAFANYA HIVYO KWA KUELEZEA TABIA YA WEMA SEPETU AMBAZO NI "UKOROFI" (DAKIKA MBILI MBELE NYUMA ), NA UKICHECHE A.K.A PASUA KICHWA (KICHWA KINAUMA)..KAMA UMESAHAU WEMA SEPETU ALIWAHI KUMTUKANA BOB JUNIOR MATUSI YA NGUONI, KESI IKAENDA MAHAKAMANI..UNAKUMBUKA HIYO?



Oyayee , mbona unawatesa sana,

HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND MBONA UNAWATESA SANA HAO WASICHANA UNAO WABADILISHA BADILISHA ?

Omamee, omame oya mame, omame oya mamee
Mbona unajitesa sana

HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND "WHAT GOES AROUND COMES AROUND". ANAVYO WATESA HAO WSICHANA, NI SAWA NA KUJITESA MWENYEWE TU. UKICHECHE WA DIAMOND UNAMTESA KIASI CHA KUMFANYA ASHINDWE KUJUA AMPENDE NANI KATIKA MAISHA YAKE, KWA SABABU WANAWAKE KARIBU WOTE ANAO TOKA WANAKUWA NA KASORO ZISIZO VUMILIKA.

Omamee, oya mame, omame oya mamee
Ukaanza kulewa, madawa kuvuta kwa sana.


HAPA ALIKIBA ANATHIBITISHA NAMNA AMBAVYO HALI YA KUWATESA WANAWAKE INAMRUDIA DIAMOND MWENYEWE. BAADA YA KUUMIZWA NA MWANAMKE/WANAWAKE, DIAMOND AKAONA HAKUNA NJIA NYINGINE YA KUPAMBANA NA MAUMIVU YA KUUMIZWA NA MWANAMKE, ZAIDI YA KULEWA. DIAMOND ALITOA WIMBO, " NATAKA KULEWA" AMBAO ULIKUWA BASED ON TRUE STORY.


Ndani ya Dar Es salaam, mambo matamu hayakukwisha hamu

HAPA ALIKIBA ANAELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND HAJAISHIWA NA HAMU YA KUTEMBEA NA WANAWAKE AMBAO ANAWAPATA BAADA YA YEYE KUWA MAARUFU KUPITIA MUZIKI.


We bado mtoto wa mama hujayajua mengi


HAPA ALIKIBA ANAUA NDEGE WAWILI KWA JIWE MOJA., KWANZA ANATOA UFAFANUZI WA MTU ANAYE MZUNGUMZIA. ALIKIBA ANATAKA UJUE KUWA ANAMZUNGUMZIA DIAMOND NA SIO MTU MWINGINE YOYOTE YULE, SO ANAELEZEA JAMBO LINALO ASHIRIA MTU ANAYE MZUNGUMZIA HAPA " we bado mtoto wa mama " DIAMOND NI MTOTO WA MAMA, YUPO KARIBU ZAIDI NA MAMA YAKE NA HANA MAWASILIANO MAZURI NA BABA YAKE. ( UKISIKILIZA VIBAYA HAPO UNAWEZA KUDHANI ALIKIBA ANA MAANISHA "MTOTO KWA MAMA", BUT KIUKWELI ANAMAANISHA "MTOTO WA MAMA" )
NA ANAPOSEMA HUJAYAJUA MENGI, ANAELEZEA MTAZAMO WAKE KUHUSU UPEO WA DIAMOND, KUHUSU MAISHA YA MWANADAMU. ALIKIBA ANA AMINI KUWA DIAMOND BADO HAJAJUA MENGI KUHUSU MAISHA, NDIO MAANA ALIWADHARAU SHAROBARO RECORDS WALIO MTOA PAMOJA NA BABA YAKE MZAZI.


Mwenda tezi na omo marejeo ngamani
HAPA ALIKIBA ANAMKUBUSHA DIAMOND ASISAHAU ALIPOTOKA.


Amesema sana mama, dunia tambala bovu

Kuna asali na shubiri ujana giza na nuru

HAPA ALIKIBA ANAMSHAURI DIAMOND, ASICHEZE NA UJANA WAKE NA AKUMBUKE KUWA KUNA WAKATI WA KILA JAMBO, LEO YUPO JUU KIMUZIKI NA KIMAISHA LAKINI KESHO ATAKUWA CHINI. SO AKUMBUKE ALIPOTOKA, ASIJISAHAU.


We mwana wewe mwana, mbona jeuri sana

HAPA ALIKIBA ANA ELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEKUWA JEURI BAADA YA KUPATA MAFANIKIO YA KIFEDHA NA KIMUZIKI.


Ulichokifata hukupata , umekosa ulivyo achaa

Kwa baba yako mwana, na mama yako mwana


Kwa vicheche ulivyo vitaka , ni vingi ulivyo achaa,



HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND " UMEKIMBIA SHAROBARO RECORDS NA KWENDA KWINGINEKO ILI UPATE UPATE MAFANIKIO ZAIDI YA KIMUZIKI NA HATIMAYE UPATE FURSA YA KUN'GOA MADEMU, LAKINI UMEISHIA KUPATA VICHECHE TU KAMA AKINA WEMA SEPETU NA JOKATE. WAKATI VICHECHE KAMA HAO ULIKUWA NA NAFASI YA KUWAPATA HATA KAMA UNGEBAKI SHAROBARO RECORDS. MATOKEO YAKE SASA, WALE MADEMU AMBAO ULIKUWA UNAWATAKA WAKATI UPO SHAROBARO RECORDS ( AMBAO WALIKUWA NA AFFILIATION NA SHAROBARO RECORDS) UMEWAKOSA NA MADEMU AMBAO ULITARAJIA UNGEWAPATA UKIWA NJE YA SHAROBARO RECORDS HUJAWEZA KUWAPATA.



Oyayee, mbona unajitesa sana

Mbona unawatesa sana

( IMESHAELEZEWA JUU )


UNALETA LAWAMA, UNALETA LAWAMA X 2
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, siku zote leilee
Analiaa oooh oooh oooh oooh
Kutwa nzima analalamika
Obaba baba na mama yako yako, oooh mwana rudi eeeh
Watafurahi wakikuona umerejea salama.


HAPA ALIKIBA AMEFANYA KAMA KUPOTEZA MABOYA VILE ILI ASIONEKANE KAMA ANAMPIGA MADONGO DIAMOND MOJA KWA MOJA.

No comments:

Post a Comment